Watunga Sera Waongo na waovu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watunga Sera Waongo na waovu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by LENGEJU BOB, Apr 13, 2012.

 1. L

  LENGEJU BOB Member

  #1
  Apr 13, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=6]Wanakitukuza kiswahili majukwaani,
  Wanakipigia chapuo vikaoni,
  Wakitumia siasani, kura wanapata,
  Watatunga sera na Kanuni,
  Kiswahili Lugha ya Taifa.

  Wanalazimisha mfumo, kifundiswe toka chekecheani,
  Nachingwea, Biharamlo, Nyandira, Ngarenanyiki, Malangali,
  shule za kata zote Kiswahili!
  Halafu watoto wao wanawapeleka “English Medium”…………………………………..

  Ni waongo, wahuni,
  wanatuhadaa, wanahujumu utu wetu
  Wanachakachua Uhai wetu!
  Wanajali wale walio kwao kuliko hawa wa huku kwetu.

  Wanafikiri, wanawazia matumbo yao,
  Hawajengi Tanzania, bali familia na koo zao,
  Kila mdosi ana jina lao,
  Wanarithishana vyeo vyao, utajiri wao, uharamia na ufisadi wao..

  Ole wao, Ole wao….
  Zinakuja siku zao,
  Watalia kwa matumbo yao
  Watasahau na Majina yao………….
  [/h]
   
Loading...