Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,683
- 2,158
Ukimsikiliza vizuri katika hotuba zake Mh. Rais ni "Kama" ana nia njema ya kutaka kujenga taifa la kistaarabu ambalo limestaarabika, lenye kuheshimiana, kujali na kuthamini utu wa mtu.
Rais anaposema watumishi wa umma wasukumwe na dhamira zao kufuata ethics anatakiwa ajue viongozi huandaliwa. Hivyo badala ya kuongea anatakiwa atende!
Rais anatakiwa aweke mkakati wa kuhakikisha viongozi na watumishi wa umma wanapata hizo refresher course na ahakikishe kweli zinawasaidia
Bahati mbaya iliyopo hata refresher course zilizopo au mafunzo kazini kwa baadhi ya watumishi wa umma hazina matokeo mazuri kwasababu ya utaratibu uliopo.
Utaratibu wa kulipa posho watumishi wa umma/ viongozi wanaopata mafunzo ya kuongeza ujuzi wao binafsi ili kuleta tija katika kazi zao ambayo ni sifa nzuri sijui ulikopwa wapi.
Watumishi wa umma/ viongozi wanapohudhuria mafunzo fulani wanalipwa allowance.
Hii huongeza gharama kwa serikali ndiomaana ziko chache na hata zilizopo zinakuja kwa kuwalenga watu walewale kwa sababu ya maslahi kiasi kwamba hata wakirudi kwenye vituo vyao vya kazi wanapata ugumu kuwafundisha wengine kwasababu ya kutokuwa na utayari
Jambo lingine ni umakini mdogo wa hawa wanapohudhuria hizo training. Si ajabu asizingatie mafunzo badala yake anasubiri siku ziishe apewe posho yake.
Binafsi sioni sababu ya wanapohudhuria mafunzo kazini kulipwa posho badala yake wanaweza hata kujigharamikia baadhi ya gharama kwasababu wakishapata ujunzi unabaki kuwa wao binafsi!
Huu utamaduni Kuna wakati unawaletea usumbufu hizi taasisi au NGOs za nje. Unakuta wakiita watu kwa ajili ya kutoa elimu ya jambo fulani kinachouliziwa kwanza huwa ni posho kuliko hata umuhimu wa kinachoenda kuelezewa.
Huu utamaduni hauna budi kurudi ulikotoka ili tupige hatua! Nchi masikini Kama yetu inahitaji watu kupeana elimu na ujuzi zaidi wa kuboresha utendaji kazi kuliko kulipana posho za kupata ujuzi
Hivyo basi, kuliko Mh. Rais kusema watumishi wa umma hawajielewi badala yake wanasubiri kufokewa ndio wawajibike anatakiwa aone haja ya kulibadilisha hili.
Ki ukweli mtu anayesubiri kufokewa ndio atende vizuri huyu hajielewi. Hii mentality inatakiwa ibadilishwe na wakuibadilisha si mwingine ni yeye.
Kiongozi wa familia ndio mbeba maono ya familia hali kadhalika kwa kiongozi wa nchi.
Yeye ndio anatakiwa aweke dira ya Taifa na watu wake. Akiliweza hili Taifa litapiga hatua ndani ya muda mfupi kwani sababu ya nchi yetu kusua sua ni kukosekana kwa viongozi wenye commitment!
Hizi refresher course anazoongelea zinaouwezo wa kuchochoe viongozi/watumishi wa umma kuwa committed na wakafanya kazi vizuri kwa kuzingatia ethics za Taaluma zao pasipo kufokewa fokewa kana kwamba bado tuko enzi za utumwa!
Kustaarabika ni pamoja na kutimiza wajibu uliopewa pasipo kushurutishwa.