Watumishi wa umma wako mbali na kujiajiri, hawana jeuri ya kuacha ajira ya serikali!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,793
Zoezi la watumishi hewa na lile la kuhakiki vyeti limenidhirishia kuwa watumishi wengi wa serikali hawana jeuri ya kuthubutu kujiajiri au kutema utumishi wa umma.
Pamoja na manyanyaso yote waliyoyapata kwenye zoezi hili, pamoja na kuhenyeshwa kukimbia huku na kule wengi wao bado wameendelea kukabembelezea hako ka ajira kana kwamba ndio kila kitu kwenye maisha.
Alafu sasa.
Ukienda ofisi za umma kudai huduma wanavyovimba na kunata utadhani wao ndio maraisi wa nchi hii. Na vitumbo vyao wamevivimbisha na kuvipamba kwa tai, kumbe hamna jeuri yeyote.
Kuanzia sasa sitishiki na mtumishi yeyote wa umma. Mbali na hako ka ajira hawana jeuri ya kuendelea kukaa hapa mjini.
Sie tuliojiajiri ndio wanaume wa shoka. Unaamka mda unaotaka na unafanya kazi zako bila presha na bado unailea familia hapa mjini.
Oyooo!
Saluti kubwa kwa wote waliojiajiri...
 
Unaamka mda unaotaka na unafanya kazi zako bila presha

Wapo wanaofurahi kuona wanaenda kaburini wakiwa wameutumikia umma wa watanzania kwa nguvu,akili na ari yao yote.
Kwenye bold, inaonekana unahusudu uvivu...
 
kama hujui watumishi wengi wanamiradi mbalimbali wamewekeza, wana bajaji, bodaboda, nyumba za kupangisha nk. sio wote lkn baadhi yao wanamiradi.
 
"Umesahau kwamba na wewe maisha yako yanawategemea... bila wao kukuungisha jiji ungelikimbia"
 
kama hujui watumishi wengi wanamiradi mbalimbali wamewekeza, wana bajaji, bodaboda, nyumba za kupangisha nk. sio wote lkn baadhi yao wanamiradi.

Wengi wa hao uliowataja wanaendesha miradi yao kwa hasara. Na utakuta hiyo miradi inategemea ajira zao kujiendesha, ngoja watoke kwenye ajira utakuta hiyo miradi yao inakufa baada ya muda mfupi.
 
*Utumishi wa umma niukimbia toka mwaka 2010 sahvi nimejiajiri na nina wafanyakazi 8 wanaoniita Boss*
 
Umeandika jambo la kweli sana ! Binafsi sijawahi kuajiriwa na serikali ya Tanzania na wala sioni kiwango cha mshahara kinachoweza kunishawishi kuajiriwa na serikali hii .
 
Back
Top Bottom