Watumishi wa umma waendelea kusota

Watumishi wa umma waendelea kusota

bne

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
1,686
Reaction score
2,023
Baada ya lile swala la uhakiki na kufwatiaji na zoezi la usimamishaji kazi kwa watumishi hao, maelfu ya watumishi hawakukubaliana na hali hiyo na kuamua kukata rufaa.

Kwa uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii umebaini kuwa wengi waliokata rufaa hadi sasa hawajapewa majibu yao hivyo kuendelea kusota mitaani hali inayotishia maisha yao kwa sasa. Mtumishi mmoja ambae ni wa kada ya uhasibu Kibaha, jina linahifadhiwa anasema kuwa huu ni mwezi wa tano tangu alipokata rufaa ya cheti chake lakini hadi sasa hajapewa majibu yake na kadiri anapofwatilia swala hilo anaambiwa asubiri.

"Ndugu mwandishi hali niliyo nayo Mungu ndiye anajua, watoto wangu shule sasa imekua shida, nyumba ndio nafukuzwa kwani nimepewa wiki hii kama sitatoa kodi basi nitolewe vitu nje, maisha yamekuwa nababaisha tu".

Mwandishi wa habari hizi alipofika utumishi alipata uhakika kuwa bado kuna watumishi ambao hawajapewa majibu yao ya rufaa na hata baraza la mitihani NECTA nalo limekiri kuwa kuna rufaa kibao ambazo bado hazijafanyiwa kazi kwa miezi zaidi ya mitano sasa. Kwa hali hii sasa tunamuomba Wazari mwenye dhamana kuingilia kati kuwaokoa wafanyakazi hawa kwani maisha yao yako hatarini.

Pia kwa balaza ni bora lizifanyie kazi rufaa hizi haraka ili kuziokoa familia za wafanyakazi hawa au serikali iruhusu mara moja hawa wafanyakazi waendelee kulipwa stahiki zao wakati balaza linaendela kuzifanyia uchunguzi rufaa zao.

Kama mtanzania sioni mantiki yoyote kwa rufaa hizi kuchukua muda mrefu kutolewa majibu sababu hili swala linagusa maisha ya watu na huko ni kuwaadhibu wafanyakazi hawa pasipo sababu za msingi.

KUNYANYASA WAFANYAKAZI WA UMMA NI KULINYANYASA TAIFA
 
AWAMU YA MAZWAZWA NA MIKURUPUKO MWENDOKASI
 
Back
Top Bottom