Watumishi sasa kuhakikiwa majina

Watumishi sasa kuhakikiwa majina

Tumechoka kudanganywa kama watoto wadogo aisee mh aliongea kwa kujiamini tumpe maximum miezi 2 ya uhakiki dar cha ajabu mpaka sasa teyari imetimia miezi 5....Tunaumia hasa sisi ambao tulishafanya usajili tumepita na kusaini mkataba ila tukaambiwa tupishe uhakiki kwanza...duu
 
mtarudi palepale niliposema kwamba,miaka hii mitano itaisha kwa kusikia na kuona mambo mengi ya ajabu,hasa kutoka vinywani kwa watu tuliokuwa tunawategemea kutuletea maendeleo,cha msingi ni kuweka kumbukumbu kwa yote yanayosemwa
 
hivi hawa wabunge wanakazi gan huko bungeni si walipgie kelele...
 
kila siku magufuli anazidi kunipa sababu ya kumchukia wakati mwanzo nilikua namkubali sana, huwezi kunikalisha mtaani muda wote huu bado niendelee kukupongeza kwa unacho kifanya
ndoo ukome[emoji2] [emoji2] [emoji23] [emoji23] walimchagua wa nn ccm hakuna jipya
 
Wamejipangaaaaaaa mwaka huuuuu wataisomaaaaaa.....imba....
 
vyeti walivyohakiki havikuwa na majina....??? au kitu gani...?
 
Tumechoka kudanganywa kama watoto wadogo aisee mh aliongea kwa kujiamini tumpe maximum miezi 2 ya uhakiki dar cha ajabu mpaka sasa teyari imetimia miezi 5....Tunaumia hasa sisi ambao tulishafanya usajili tumepita na kusaini mkataba ila tukaambiwa tupishe uhakiki kwanza...duu
We kaa unyoshe na miguu kabisa bado uhakiki Wa jinsia
 
Baada ya hapo kutakuwa na uhakiki wa vyeti vya kuzaliwa maana inasemekana Luna watumishi wengi tu si RAIA na walisoma hku na kupata mikopo vyuoni kwa kufoj vyeti vya kuzaliwa
 
Yes baala ya hapa watahakiki blood group na ukubwa wa makalio
 
wanajadil maadil ya wafanyakaz,hawajadil maslah ya hao wanao taka wawe na maadili! oops h nch ya kusadikika! tambua unaemtawala anawaza kama we2 na mtawala wako,humtawali mbuz tambuen hlo! hakuna kiongoz ktk nch ya kusadikika bali n mtawala. madhara ya utawala yataonekana.
 
Wao serikali ndio wanajua nia yao I think itakuwa ni nia njema
Washajua mkulu anapenda uhakiki ndio maana wanaona kiki yao ya kubaki kazini ndio hiyo.
Zikimalizika document wataanza kuhakiki mpaka jinsia za watumishi wa umma
 
SERIKALI imesema uhakiki wa watumishi wa umma, utakamilika ndani ya mwezi huu, hivyo nafasi zilizoachwa wazi baada ya kuondolewa kwa watumishi hewa, zitaanza kujazwa.

Aidha, imesema kwamba baada ya uhakiki huo ambao utasaidia kuwa na orodha sahihi ya watumishi waliopo katika taasisi za umma kwa lengo la kuboresha hali ya utumishi nchini, itaanza mfumo wa kuhakiki majina mapya.

Akizungumza katika awamu ya pili ya kipindi cha Tunatekeleza kinachorushwa TBC 1 juzi, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurean Ndumbaro alisema uhakiki wa watumishi hewa, umesaidia kuongeza ufanisi katika taasisi zake.

Dk Ndumbaro alisema baada ya kukamilika kwa uhakiki huo, pia wataanza mfumo mwingine wa kuhakiki majina mapya ambayo yatajitokeza mara mbili na kuyatoa ili kubaki na majina sahihi.

“Kwa mfano, yupo mtu anatumia majina matatu lakini akatokea mmoja akaondoa lile la katikati na kubaki na majina mawili labda Laurean Ndumbaro hivyo mfumo utaona kuwa ni jina jipya kumbe kuna mtu ambaye amejitengenezea jina hilo,” alisema Dk Ndumbaro na kufafanua kuwa ili kuondoa mkanganyiko huo, mfumo utatambua na kuyaondoa majina yasiyohusika.

Chanzo: HabariLeo =>12/10/2016
 
Back
Top Bottom