Watumishi idara ya afya wahamishwa bila malipo Tabora

Mafunguo 88

Senior Member
Dec 21, 2016
155
184
Hivi karibuni manispaa ya Tabora imepokea Daktari mkuu wa manispaa Dr Yombo baada ya alie kuwapo awali Dr Rashidi Mfaume kuhamishiwa katika mkoa wa Shinyanga.

Mara baada ya kufika na kuripoti amezungukia baadhi ya zahanati na vituo vya Afya vinavyopatikana katika manispaa ya Tabora.

Baada ya hapo aliitisha kikao cha dhalara baina yake na waganga wafawidhi wa vituo kisha kujadiliana kero na changamoto zilizo katika vituo.

Changamoto zilizoibuliwa ktk kikao hicho ni pamoja na uchache na upungufu mkubwa wa watumishi katika zahanati mbali mbali ambapo baadhi ya zahanati zina watumishi wawili ama watu kitu kinachofanya kazi za zahanati kufanyika kwa ugumu mkubwa na watumishi kukosa hata mda wa kupumzika kwa kufanya kazi masaa 24.

Changamoto nyingine wauguzi kutopewa pesa za kununua uniform kwa mda wa miaka minne sasa na pesa hiyo kutojulikana ilikopelekwa.

Pamoja na hayo Daktar huyo aliahidi kuvipanga vituo upya kwa kuwabadilisha baadhi ya watumishi vituo vyao vya kazi bila kujali upungufu wa watumishi katika vituo.

Hata hivyo mtumishi unapohamishwa kituo cha kazi unapaswa kupewa pesa ya kujikim ili ikuwezeshe kuhamisha mizigo na familia kwenda katika kituo chako kipya ila yeye amehidi kuwahamisha watumishi bila kuwalipa pesa ya aina yoyote.

Ninachojiuliza hivi kitendo hiki sio ukiukwaji wa sheria?

Na kwanini yeye kama DMO asishilikiane na afisa utumishi kuwasaidia watumishi hawa pesa za uhamisho?

Kwanini Hasikilizi ushauri anaopewa na bodi ya Afya ya Manispaa ambayo imeundwa na waratibu wa vitengo mbali mbali kuhusu kusubiria ajira mpya ili aweze kuziba mapengo ya watumishi kule wanakohitajika?


Naibu waziri wa Wizara ya Afya Jinsia wazee na Watoto tunakuomba uje utatue utata huu watumishi wa afya Tabora wanaonewa NB Upo humu na nitakutumia habari hii DM.
 
Back
Top Bottom