Watumishi hewa adui wa Tanzania ya viwanda

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
KUANZIA jana (Juni 16, 2016) Tanzania inaadhimisha Wiki ya Utumishi wa Umma barani Afrika ili kutambua umuhimu wa watumishi. Maadhimisho hayo ya kila mwaka yatakwisha Juni 23, 2016. Wiki ya Utumishi wa Umma ni miongoni mwa matukio muhimu katika kalenda ya Umoja wa Afrika (AU). Kaulimbiu katika maadhimisho ya mwaka huu ni ‘’Uongozi wa Umma kwa ukuaji jumuishi kuelekea katika Afrika tunayoitaka’’.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Angella Kairuki anasema, pamoja na kaulimbiu hiyo, maadhimisho hayo yatakuwa na dhana mbalimbali. Anasema, dhana mojawapo ni mchango wa utumishi wa umma katika ukuaji wa uchumi barani Afrika. Nyingine ni mchango wa utumishi wa umma katika kuiwezesha ajenda ya Afrika ya mwaka 2063 inayoweka mkazo katika maendeleo ya Afrika na haki za wanawake.

Anasema, maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yamekuwa yakifanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam kila mwaka kwa watendaji, taasisi na Wizara kuweka mabanda ili wananchi watembelee. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, mwaka huu maadhimisho hayo yatafanyika kwenye kila idara na taasisi. Anasema, watendaji wakuu katika Wizara, idara, mawakala na taasisi za serikali watatakiwa kutenga siku moja ya kukutana na watumishi katika sehemu zao za kazi kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi.

Watendaji wakuu wanapaswa kutenga siku moja kwa ajili ya kusikiliza kero za wananchi zinazohusiana na huduma zinazotolewa. Waziri Kairuki anasema, mikakati ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, imewekwa katika uchumi wa viwanda uliozingatia maendeleo ya watu. ‘’Kaulimbiu ya mwaka huu ya wiki ya utumishi wa umma inaendana na malengo ya serikali ya awamu ya tano kwamba i n a h a k i k i - sha kuwa Tanzania inakuwa na uchumi wa v i - wanda,’’ anasema Kairuki.

Tanzania imejiwekea malengo mahsusi ya kupiga hatua katika ukuaji wa uchumi kupitia maendeleo ya viwanda. Kairuki anasema, ili serikali iweze kufikia azma hiyo, watumishi wa umma wana wajibu wa kuwezesha wananchi kushiriki katika shughuli za uzalishaji kukuza uchumi. Watumishi wa umma wana majukumu ambayo serikali inatarajia wayafanye.

Watumishi wa umma wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii, maarifa na weledi kwa kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake waendane na kasi ya Rais Magufuli. Waziri Kairuki anasema, watumishi wa umma pia wana jukumu la kuhakikisha kuwa wanatoa huduma kwa wananchi kwa wakati, bila urasimu wala ukiritimba. Anasema, kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano inapambana na rushwa, watumishi hao wanatakiwa kuepuka vitendo vya rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao ili kutenda haki.

Watumishi wanapaswa kufanya kazi kwa kujali matokeo na wabadilike kulingana na mazingira ya wakati husika. Kairuki anasema, watumishi wanatakiwa kuepuka vitendo vya wizi, ufisadi na udanganyifu vinavyosababisha upotevu wa fedha za serikali. ‘’Tutaweza kufikia dhana ya kuwa na Tanzania ya viwanda endapo watumishi wa u m m a watafuata k a n u n i hizo na kutimiza majukumu yao kikamilifu,’’ anasema.

Waziri Kairuki anasema, serikali itaendelea kuhakikisha kuwa kuna uwiano wa jinsia katika nafasi na fursa katika utumishi wa umma ikiwemo ajira, uteuzi wa nafasi za uongozi, mafunzo kazini na upandishwaji vyeo. Viwanda kutoa ajira Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, anasema mwaka 1961, Tanganyika ilirithi viwanda 125 tu kutoka serikali ya kikoloni.

Waziri huyo mwenye jukumu la kutekeleza ahadi ya Rais John Magufuli ya kuiwezesha Tanzania kuwa nchi ya viwanda, anasema, idadi hiyo ya viwanda ni ndogo ikilinganishwa na viwanda vya sasa. Kwa mujibu wa Waziri Mwijage, hadi mwaka 2005, wakati Serikali ya Awamu ya Nne ilipokuwa ikiingia madarakani, viwanda vilikuwa vimeongezeka na kufikia 5,153.

Takwimu zinaonesha kuwa, kuanzia mwaka 2005, kasi ya kuongezeka kwa viwanda ilikuwa kubwa kuliko wakati wowote katika historia ya nchi. Kwa mujibu wa takwimu hizo, hadi kufikia mwaka 2013 viwanda viliongezeka na kufikia 49,243. Wakati wa kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu, Dk Magufuli aliwahi kusema kuwa atahakikisha anafufua viwanda 37 vilivyokufa. Kati ya viwanda 106 vilivyobinafsishwa, 45 vinafanya kazi vizuri; 24 vinasuasua na 37 vimefungwa.

Serikali ina dhamira ya kuhakikisha kuwa, viwanda vyote vilivyobinafsishwa vinafanya kazi. Waziri Mwijage anasema, kati ya viwanda 49,243 vikubwa, vinavyotoa ajira kuanzia watu 100 na kuendelea ni 247. “Viwanda vya kati vinaajiri kati ya watu 50 na 99 ni 170, viwanda vidogo vinavyoajiri kati ya watu watano na 49 ni 6,907 na viwanda vidogo sana vinavyoajiri chini ya watu watano ni 41, 919,” anasema Mwijage.

Kuhusu ufufuaji wa viwanda 37 vilivyokufa, Mwijage anasema mpango wa Serikali ni kuhakikisha viwanda hivyo vilivyofungwa baada ya kubinafsishwa, vinafanyiwa tathmini haraka kabla ya nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha unaoanza Julai Mosi mwaka huu. Kwa mujibu wa Waziri Mwijage, hatima ya viwanda visivyofanyakazi kwa sasa ipo kwa wamiliki kwa kuwa wamepewa kazi ya kutekeleza mikataba waliyoingia wakati walipouziwa na wakishindwa, viwanda hivyo wapewe wawekezaji wapya waviendeshe.

Anasema, katika kuijenga Tanzania yenye uchumi wa viwanda kuna umuhimu wa kuhamasisha sekta binafsi ya Watanzania na wageni kuwekeza kwenye sekta ya viwanda vidogo, vya kati na vikubwa. Watumishi hewa Waziri Kairuki anasema, watumishi 12,246 wameondolewa kwenye mfumo wa malipo ya mishahara kwa sababu mbalimbali ikiwemo umri wa kustaafu kwa lazima, kufukuzwa kazi, vifo na kumalizika kwa mikataba.

Anasema, kuondolewa kwa watumishi hao kumeiwezesha serikali kuokoa Sh bilioni 25 ambazo zingelipwa kwa watumishi hao kwa mwezi Mei mwaka huu. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, fedha hizo zingepotea endapo watumishi wasingeondolew a kwenye mfumo ikilinganishwa na watumishi 10.295 walioondolewa kwenye mfumo kuanzia Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu.

Anasema, watumishi hewa 4,317 walifutwa baada ya kufanya uhakiki katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia Machi mosi hadi Aprili 4, mwaka huu. Watumishi 3,033 waligundulika mara tu baada ya Rais Magufuli kutoa tamko Machi 15 mwaka huu. “Jumla ya Sh bilioni 23.2 ziliokolewa kwa kipindi cha Machi 15 hadi Aprili 30 mwaka huu baada ya Rais Magufuli kutoa maagizo ya kuwaondoa watumishi hao kwenye malipo,” anasema Kairuki.

Anasema, watumishi hewa 1,951 wameongezeka ikiwa ni Sh bilioni 1.8 zimeokolewa. Waziri Kairuki anasema, makatibu wakuu, wakuu wa taasisi za umma na mamlaka za serikali za mitaa walitakiwa hadi Juni 10 mwaka huu wawe wamewasilisha taarifa za watumishi hewa. Kairuki anasema, taarifa hizo zinatakiwa zibainishe majina, namba za hundi za watumishi hewa, tarehe walizotakiwa kuondolewa kwenye mfumo, tarehe walizoondolewa, kiasi cha fedha kilichopotea na kilichookolewa.

Anasema, taasisi nyingi zimewasilisha taarifa hizo na zimefanyiwa tathmini ili kupata uhakika namna shughuli hizo zilifanywa. Kairuki anazitaka taasisi zilizobaki ambazo hazikutoa taarifa hizo kutoa taarifa na kwamba wahakikishe wanaziwasilisha.

Anawataka makatibu wakuu, makatibu tawala wa mikoa na wakuu wa taasisi za umma na mamlaka za serikali za mitaa kufanya tathmini ya uwepo wa watumishi hewa na kutoa mapendekezo ya namna ya kuondokana na changamoto hiyo.
 
Back
Top Bottom