Watumishi feki njiapanda

Faru fausta

JF-Expert Member
Apr 29, 2017
218
143
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Dk Yahya Msigwa

Dar es Salaam. Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (Tucta), Dk Yahya Msigwa amesema wafanyakazi wa umma 9,932 waliobainika kuwa na vyeti bandia wakiacha kazi kwa hiari watakuwa wamekosa viinua mgongo vya miaka waliyoitumikia Serikali.

Ijumaa iliyopita, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angellah Kairuki alimkabidhi Rais John Magufuli ripoti ya majina hayo ambayo yameibua mjadala mitaani na mitandaoni.

Akizungumzia suala hilo, Dk Msigwa amesema kama watumishi hao wataendelea kubaki kazini watashtakiwa kwa kughushi vyeti na kujipatia mshahara kinyume na sheria.

“Hapa kuna mtego wahusika wenyewe wataamua kama waendelee na kazi ili waje washtakiwe au kujiondoa mapema na kuacha kiinua mgongo chao,” amesema katibu huyo.

Kwa mujibu wa Sheria ya Kazi na Uhusiano Kazini namba 6 ya mwaka 2004, mwajiri anawajibika kumlipa haki zake mfanyakazi pale anapomwachisha kazi.

Hata hivyo, Dk Msigwa amesema Serikali ikiamua kuwafukuza kazi kwa sheria hiyo ni lazima walipwe stahiki zao kwa sababu wameondolewa kwenye ajira kwa lazima.

“Kwa sheria ya kazi namba sita (ya mwaka 2004) hakuna neno kufukuzwa kazi, ukimwondoa kazini mtumishi ni lazima umlipe kiinua mgongo, ndiyo maana hapa ninaona agizo la Rais Magufuli ni mtego ili waache kazi wenyewe,” alisema.

Baada ya kupokea ripoti hiyo, Rais Magufuli aliwataka wafanyakazi hao kuacha kazi ndani ya siku 15 vinginevyo wakumbane na mkono wa sheria baada ya kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwachukulia hatua.
 
Ingawa kufoji vyeti ni kosa, lkn waliofoji wamefanya kazi kwa ufanisi. Sijasikia serikali inalalamika kuwa hawa waliofoji vyeti wameitia hasara serikali.. Kwa msingi huu nasema serikali inafanya uharamia wa kutaka kuiba pesa za watu. Hii ni Dhambi kubwa.
 
Kwani hayo maagizo kuna mtumishi aliyeandikiwa barua? Mtumishi anaajiriws kwa barua anaondolewa kwa barua sio matamko. Serikali ndio utakayolianzisha kwa kusimamisha mishahara.
 
Hivi kuwa na cheti halali inashindikanaje mpaka ufoji??
Shule kipaji mkuu
Kwa tafsiri yangu: Kipaji ni uwezo wa kipekee anaokua nao mtu flani na uwezo huo unamuwezesha kufanya jambo flani kwa usahihi kuliko watu wengine.

Kuna watu hata wakeshe wanasoma, wakiingia chumba cha mtihani kila kitu wamesahau
Mtihani uheshimiwe na kila mweye pumzi

Ingawa kufoji vyeti ni kosa, lkn waliofoji wamefanya kazi kwa ufanisi. Sijasikia serikali inalalamika kuwa hawa waliofoji vyeti wameitia hasara serikali.. Kwa msingi huu nasema serikali inafanya uharamia wa kutaka kuiba pesa za watu. Hii ni Dhambi kubwa.

uNAIBIWAJE PESA WAKATI C PESA YAKO YA HALALI? KAMA UMEFOJI VYETI WEWE NDIO MWIZI UMEIIBIA SERIKALI UNATAKIWA KURUDISHA PESA ZOTE.
 
Shule kipaji mkuu
Kwa tafsiri yangu: Kipaji ni uwezo wa kipekee anaokua nao mtu flani na uwezo huo unamuwezesha kufanya jambo flani kwa usahihi kuliko watu wengine.

Kuna watu hata wakeshe wanasoma, wakiingia chumba cha mtihani kila kitu wamesahau
Mtihani uheshimiwe na kila mweye pumzi

KAZI KWELIKWELI...KWELI MTIHANI UHESHIMIWE
 
Back
Top Bottom