Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,563
- 21,665
Watuhumiwa wawili wanaodaiwa na kujihusisha na mtandao wa kutengeneza bima feki wamekamatwa katika msako unafanywa na wakaguzi kutoka ngazi mbalimbali kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani Arusha na baadhi ya wananchi walioathiriwa na mtandao huo.
Wananchi hao wakiwemo Madereva wamesema hatua ya kutakiwa kulipia tena Bima za Magari yao baada ya kukamatwa na kubainika kuwa ni feki ni uonevu na hasara isiyo ya lazima na kwamba serikali ingetakiwa kuwajibika kwani kwa upande mwingine ndiyo inachangia kuwepo kwa mianya wanayotumia matapeli hao.
Meneja wa Shirika la Bima kanda ya Kaskazini Bi.Stela Rubaguza amesema watuhumiwa hao wamekamatwa katika wilaya ya Karatu ambayo asilimia kubwa ya stika za bima zimebainika kuwa ni za bandia.
Kwa upande wao baadhi ya wadau wakiwemo wamiliki wa vyombo vya moto wamesema tatizo la bima za feki ni kubwa zaidi katika maeneo ya vijijini ambako licha ya wananchi kukosa uelewa pia hakuna ukaguzi wa mara kwa mara.