Zimpombe
Member
- Aug 9, 2016
- 28
- 24
"We are not obliged even the last to prove to anybody and to the black that we are superior people. We have demonstrated that to the Blacks in southands and one ways". Kauli hii sio tu kwamba inanitweza utu wangu kama mtu mweusi, bali inaongelea ukweli ambao ni mchungu kuumeza. Pieter Willem Botha, nani angeweza kumpinga kwa hoja zenye ujazo pasipo kuweka mbele hoja ya kuwa tunabaguliwa? Sizipendi kebehi hizi; sifurahii dharau hizi, inatupasa kupinga kwa vitendo chanya kuwa mtu mweusi ni bora, sio kwa maandamano wala historia, maana historia ni kumbukumbu tu iliyo ganda kama jiwe.
Mwingine alienda mbali zaidi, akasema " Africans are lazy, fools, only good at eating, lovemaking and thuggery". Niliumia sana kwa kauli hii hata kama si Trump aliongea, lakini ujumbe ulifika. Nilijiuliza sana hivi sisi watu weusi tunalaana gani ambayo wazungu wanaiona ila sisi tunashindwa kuiona?
"The fact that Blacks look like human beings and act like human beings do not necessarily make them sensinsible human beings". Shit!! Hivi huyu Botha, mbona alikuwa anaongea maneno mazito kuyameza? Yaani mamba sio mamba; kenge sio kenge, sijui ni nini eti! Nimesikia na yule wa Israel kaongea maneno ya kashfa, sijajua kama kweli. Lakini kosa letu nini hasa?
Baada kukaa chini na kutafakari, niligundua mzungu sio mnafiki kama alivyo mtu mweusi. Mzungu njano husema njano, nyeusi husema nyeusi. Sisi watu weusi hususani kutoka Afrika, tumejawa unafiki mkubwa- nyeusi husema njano; njano husema nyeusi. Botha ama Trump ni watu wa mfano ambao wametueleza ukweli udhaifu wetu ili tuumie na kuamka usingizini.
Ni viongozi weusi ambao huiziibia nchi zao na kuhifadhi fedha ktk benki za Ulaya ili kuwanufaisha wazungu. Ni afrika pekee ambako viongozi hutunga Sera mbovu za elimu, ili wananchi wao wawe vilaza wasiweze kuhoji nakufanikisha 'smooth rule' ilihali watoto zao wakisoma nje ili waje kuongoza wajinga. Mfano, daraja muhimu lakuzalisha werevu, yaani waalimu, wanachukuliwa walio feli. Ni sisi watu weusi tukipewa silaha tutauana kama mbwa, nahata hatujui tunauana kwa nini.
Hivi Mungu ametunyima nini? Mbona tunakuwa sana omba omba kama Matonya? America, Israeli, Ufaransa, China tuzaziomba leo zimejenga uchumi wao kwa jasho, damu na maumivu makubwa. Kwanini sisi tunakuwa na 'simple mind kama bata? Ndio, kazi yetu kuoa wake wengi, kufanya mapenzi na kujisifu kupiga mabao mengi, kula vitavitamu, kuiba, kuvaa, majungu na kucheza tu.
Viongozi wa kiafrika; wa kileo, hawana ubunifu wa kuweza kuleta maendeleo ilihali utajiri wameukalia. Kazi yao nikufuga vitambi, kuwagawanya wananchi kwa kutumia uchama, kuwatisha wananchi wanapokosoa. Ndio hawa waliofanya elimu kuwa dhaifu ili watawale vizuri wakati huo wazungu wakijitahidi kuboresha elimu wakijua ndio msingi wa maendeleo.
Ni Afrka tu ambako bunge linakuwa sehemu yakuchambana na kusutana. Sijui. Labda kwa kuwa mabunge yetu wanaingia vilaza. Wabunge wanajadili maisha ya watu binafsi badala ya maslahi ya taifa.
Watu weusi tumekuwa wamapokeo tu. Dini zenyewe mapokeo alafu leo weusi wauana kwayo. Jiulize kama Yesu, au mtume Muhamad angekuwa mweusi; Ni mweupe gani angejipendekeza kusujudu?
Ni Afrka ambako viongozi hawaheshimu katiba na kujifanya miungu watu. Amri inatoka kwa mtu mmoja, hata taasisi hazina nguvu zinakuwa kama toi tu.
Leo hii mpe mwafrika hata uwanja mpya wa mpira, kesho atakunya juu ya viti, atang'oa viti na masinki ya choo. Hapa lawama ziende kwa viongozi walio waliotunyima elimu bora nakutufanya wajinga ili watutawale, na haya ndiyo madhara yake.
Hivi kweli tumelaaniwa? Sitaki kuamini!