Watu weupe huenda wakanufaika zaidi na serikali ya Magufuli

GadoTz

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
350
569
Wakati serikali ya Magufuli ikipiga marufuku uingizaji wa bidhaa za nje na kujitahidi kuweka mazingira ya kulinda bidhaa za ndani.

Kuna mambo mawili makubwa yatatokea ndani ya miaka 10 ya utawala wa Magufuli.

Watu weupe haswa wahindi na waarabu wataigeuza hiyo ni fursa na kuwekeza zaidi kwenye sekta zitazolindwa soko lake. Tutaona wakianzisha viwanda vya vidogo na vya kati.

Mfano mpaka sasa nimeshuhudia rafiki zangu wawili wa kihindi mmoja ameagiza vifaa kwa ajili ya kuprocess asali. Na mwingine anapambana kufungua kiwanda cha mifuko ya karatasi na vibebeo vya karatasi hapa hapa Dsm juzi alikuwa mufindi kuna kiwanda cha karatasi kuna vitu alienda kuweka sawa.

Upande wa pili ni sisi waswahili.

Sisi hii sera mpya aliokuja nayo Magufuli tutaitumia kama excuse nyingine ya kushindwa kwetu kwenye maisha.

Waandishi wa habari wataandika sana makala za kumkosoa asubuhi na mchana. Wanasiasa watatuimbisha kwenye majukwaa ubaya wa hii sera, tutambiwa rais hana nia nzuri na sisi, anataka sifa, anakurupuka nk nk.

Wananchi tutalalamika sana mbona viwanda vyenyewe hatuvioni.. Wakati tunatengenezewa fursa ya kuanzisha ata vya kwetu vidogo vidogo.

Nimesikia juzi Waziri anampa sifa mbunge Lema kwa kuagiza mtambo wa kutengeneza toothpick, big up kwake badala ya kulalamika tu amechukua hatua... Na ingekuwa vizuri atoe elimu kwa wananchi nini maana ya Tanzania ya viwanda.

Mwisho wa siku baada ya miaka tukianza kuhesabu tumenufaika nini na serikali ya Magufuli. Weupe watazidi kuwa mbali, sisi ngozi nyeusi tutahesabu lawama tulizotupa kwa serikali na stress tulizojipa.
 
Siamini kama ni watu weupe tu ndo watafaidika na viwanda, sema wenye akili na mitaji ndo watafaidika na sera ya viwanda. Mtu asiyekuwa na kitu akimshauri mwenye kitu - ushauri wake unaonekana wa kijinga ... haya nimeyaona na ninaendelea kuyaona. Tunaposema kiwanda sio lazima kiwe kiwanda kikubwa chenye kuhitaji mtaji mkubwa sana, nimewaona watu wakianzisha viwanda vidogo vya kusindika juice na vimesimama lakini shida ikawa ni ushindani toka bidhaa hizo toka nje ya nchi.
Ombi kwa serikali: Weka mazingira mazuri na raisi kwa wenye kuhitaji mitaji midogo na yakati kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo, vya kati. vikubwa yatakuwa matokeo tu.
 
Una point. waswahili tuamke, tuache kutumika tumika. Kama unafikiria kitu cha kufanya, anza sasa kufanya usisubiri mtu au kesho ndo ufanye.
Mfano nahitaji kuanzisha kiwanda cha sabuni .... mtaji shida ... ukienda benki - longolongo ... wakopeshaji binafsi hawaingiliki .. utaanzaje leo?
 
Huo ndio ukweli, kila wakati akili zetu zinatoa sababu za kwanini haiwezekani badala ya kwanini inawezekana. Tunapenda vitu vizuri na tunapenda vitokee tu, tuvikute tu....African mentality
 
Siamini kama ni watu weupe tu ndo watafaidika na viwanda, sema wenye akili na mitaji ndo watafaidika na sera ya viwanda. Mtu asiyekuwa na kitu akimshauri mwenye kitu - ushauri wake unaonekana wa kijinga ... haya nimeyaona na ninaendelea kuyaona. Tunaposema kiwanda sio lazima kiwe kiwanda kikubwa chenye kuhitaji mtaji mkubwa sana, nimewaona watu wakianzisha viwanda vidogo vya kusindika juice na vimesimama lakini shida ikawa ni ushindani toka bidhaa hizo toka nje ya nchi.
Ombi kwa serikali: Weka mazingira mazuri na raisi kwa wenye kuhitaji mitaji midogo na yakati kwa ajili ya kuanzisha viwanda vidogo, vya kati. vikubwa yatakuwa matokeo tu.

Ni kweli kuna mazingira bado magumu kwenye uwekezaji kwa wenye mtaji mdogo ila pia kuna uzembe kwetu sisi waswahili.

Mfano ukisikia serikali inapigania usafi mjini ujue hiyo tayari ni fursa. Unaanza kujipanga ni namna gani naweza kuitumia.

Kwa hili wenzetu wametuzidi sana, huwasikii wakilalama hovyo ni kuchangamkia fursa tu.
 
Naunga mkono hoja 1000%. Wenye mitaji ambao wengi ni Wahindi ndio watafaidika na sera hii ya viwanda. Mapesa yaliyofichwa Panama sasa yatakuja kuanzisha viwanda na waswahili tutabaki vibarua tu.
 
Mfano nahitaji kuanzisha kiwanda cha sabuni .... mtaji shida ... ukienda benki - longolongo ... wakopeshaji binafsi hawaingiliki .. utaanzaje leo?

ungana na wezako katika vikundi, inakuwa laisi kukopesheka, kama tutaendekeza kulaumu na kulalamika, alichosema mleta maada ndicho kitakacho tokea. kalime hata matikiti hekali moja baada ya hapo utapata mtaji wa biashara unayoipenda.
 
Mie Ninampango Wa Kufungua Kiwanda cha Kupack Asali Uku Meatu!Nyuki ni Wengi na Wanaishia Kuuma Watu Tu!
Nimeshaanza na Mwakani Naongeza Mizinga ya Nyuki"
 
Naunga mkono hoja 1000%. Wenye mitaji ambao wengi ni Wahindi ndio watafaidika na sera hii ya viwanda. Mapesa yaliyofichwa Panama sasa yatakuja kuanzisha viwanda na waswahili tutabaki vibarua tu.
Watu wa hisabati njooni mnisaidie hapo kwenye red bold
 
ungana na wezako katika vikundi, inakuwa laisi kukopesheka, kama tutaendekeza kulaumu na kulalamika, alichosema mleta maada ndicho kitakacho tokea. kalime hata matikiti hekali moja baada ya hapo utapata mtaji wa biashara unayoipenda.
Swali langu ni UTAANZISHAJE LEO?
Maelezo yako yako sahihi mkuu
 
Naunga mkono hoja 1000%. Wenye mitaji ambao wengi ni Wahindi ndio watafaidika na sera hii ya viwanda. Mapesa yaliyofichwa Panama sasa yatakuja kuanzisha viwanda na waswahili tutabaki vibarua tu.

umemuelewa ila umeshindwa kupambanua lengo lake, lengo lake ni waswhili tuamke tuache kulalamika na kuendekeza siasa, tuitumie fursa hii, utasema huna mtaji lakini unamiliki simu ya laki na nusu, kwanini usifuge kuku baada ya miaka miwili umeshapata mtaji wa kununua mashine ya kusaga unga nu ya kufungasha viroba vya unga. kiwanda sio lazima uwe mtambo mkubwa.
 
waswahili kazi zao ni ku manage mifugo/maandazi/vitumbua.kiwanda ni habari ya weupe.
we mweupe au mweusi?

ok, kumbe unaongelea management??? hapo sawa - nilitaka nikupe mifano ya viwanda vinavyomilikiwa na weusi ila menegement ni weupe
 
Thread nzuri sana, inafikirisha. Wahindi wanajua sana kuishi kwa kubana matumizi. Mswahili siku zote anataka afanye kazi ndogo halafu apate kingi ambacho hakilingani na jasho lake. Wengi wetu ni wavivu wa kufikiri kama alivyowahi kusema mzee BWM, tunao uwezo mkubwa wa kukosoa, kutukana, kulaumu na upuuzi mwingine wa aina hiyo.
 
KATIKA HILI NAKUUNGA MKONO ...
 
Mfano nahitaji kuanzisha kiwanda cha sabuni .... mtaji shida ... ukienda benki - longolongo ... wakopeshaji binafsi hawaingiliki .. utaanzaje leo?
Weka mikakati tofauti ya namna ya kupata mtaji siyo uweke mayai kwenye begi moja. Plan A ikigoma nenda plan B etc. Sasa ukikaa tu kusema benki longolongo huwezi kupata mtaji. Ongea na watu, utapata mawazo na sehemu ya kupata mtaji. Zichukulie kama changamoto za kukabiliana nazo kufikia kwenye malengo yako.
 
Una point. waswahili tuamke, tuache kutumika tumika. Kama unafikiria kitu cha kufanya, anza sasa kufanya usisubiri mtu au kesho ndo ufanye.
Tatizo lipo hapa mswahili ukienda bank na kuomba mkopo hupewi. Kama utapewa basi uwaweke rehani ukoo wako mzima. Lakini hao sunche samche wakifika bank tu wana nyenyekewa kama sijui nani.
 
Back
Top Bottom