Tutor B
JF-Expert Member
- Jun 11, 2011
- 9,025
- 6,618
Kwenda shule ni ile hali ya kuhudhuria kwenye kituo kinachojishughulisha na kutoa elimu. Watu wengi wameenda shule .. iwe ya msingi, upili, vyuo n.k. Ila ni wachache sana ten asana walioelimika. Nini sababu?
Ili uelimike, jambo la kwanza ni lazima uwe umejiandaa kifikra. Fikra za mtoto zinawaza michezo na ndiyo maana anamudu michezo mingi kuliko masomo darasani. Hivyo watoa elimu kwa watoto wazingatie hilo … wawatengenezee watoto mazingira ya kuchanganya kile wanachojifunza kujumlisha na kile wanachokiweza na kukipenda.
Nikija kwa watu wazima, hawa wanajifunza vitu ambavyo haviko kwenye fikra zao .. ni raisi mtu kujifunza kwa kuona, kusikia kuliko kumfundisha kitu ambacho yeye mwenyewe anakiona hakina manufaa kwake. Hii inasababishwa na kasumba ya kupenda kuiga. Ili kasumba hii iondolewe kwenye fikra za watu, inabidi kila mtu atengeneze mazingira ya kufanya mambo mapya au kurekebisha yale yaliyopo.
Kila siku binafsi nalia na mfumo wa elimu yetu hapa Tanzania. Tumekuwa na kasumba ya kuiga tu kwa wale waliotuzidi kifedha. Utamkuta mtu anasema “NATAKA MWANANGU ASOME SHULE ANAYOSOMA MTOTO WA FULANI” … hajiulizi kile kinachofundishwa kule ni nini? Hivi hiyo ada unayoitoa kwa mwezi, ukiiongeza kwa mfanyakazi wako wa ndani akawa anamfundishia hapo nyumbani hataweza kuelewa? Kule kuiga kwa jirani ndo kunafanya watoto wetu wakose elimu au wapate elimu isiyoendana na mazingira tunayoyaishi. Elimu ianzie nyumbani – mtaani – katani .. ndo twende kwenye ngazi za juu.
Wale waliotutangulia kielimu hawawezi kumwajiri mfanyakazi wa ndani kwa ajili ya kazi moja tu ya kuosha vyombo, kusafisha vyoo na kupika tu. Wafanyakazi wa ndani wenye elimu ya kufundisha watoto wachanga ndo wana soko kubwa kwa wenzetu. Lakini kwa hapa Tanzania unamkuta mtu eti anaenda kijijini kutafuta mfanyakazi wa ndani (hajui kusoma, kuandika, kuhesabu n.k.) – hii ni kudumaza elimu.
Matendo yako kwenye jamii ndiyo yanayoonesha kiwango chako cha elimu uliyo nayo - siyo makaratasi uliyopewa toka kwenye vituo ulikokwenda kupoteza muda wako na pesa za wafadhili wako.
WEWE ULIYEENDA SHULE WAKATI HUJAELIMIKA CHUKUA HATUA.