Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,411
Watu wawili wakazi wa vijiji vya Mawanjeni wilaya ya Moshi na Westkilimanjaro wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wamejeruhiwa vibaya na Nyati na kulazwa katika hospitali ya rufaa mjini Moshi.
Majeruhi hao Bw Andrea Maole amelazwa katika chumba cha wagonjwa mahututi huku akiongea kwa shida amesema,tukio hilo lilimtokea wakati akiwa shambani kwake akirejea nyumbani.
Amesema,wakati akiwa shambani aliwasikia mayowe ya watoto wake wakipiga kelele za “Nyati Nyati” na ghafla alijikuta akivamiwa na nyati mmoja kati ya nyati watatu ambao ni dume,jike na mtoto.
Majeruhi mwingine Bw Mashaka Julius mkazi wa Westkilimanjaro amesema, nyati hao ambao wanarandaranda kutoka wilaya za Rombo,Moshi na mwingine wa Siha alikutana na Nyati baada ya kutoka shamba akielekea nyumbani na kuanza kumshambulia ingawa alikimbia bila mafanikio.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Dr Hanson Nkini amesema,majeruhi wote wanaendelea vizuri na Bw Maole ambaye aliumizwa zaidi amefanyiwa oparesheni.
Afisa ardhi na maliasili wa wilaya ya Moshi Bw Msami Mshana amesema, baada ya kupata taarifa za nyati hao juhudi zimeanza kupambana nao katika vijiji vya kata ya Kilema Kusini kwa ushirikiano na maafisa kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (kinapa) na Idara ya wanyamapori Kanda ya Kaskazini.
Chanzo: ITV