The redemeer
JF-Expert Member
- Jan 28, 2025
- 4,780
- 8,160
.
Nakusalimu katika jina la Bwana Yesu Kristo alitupa neema ya kuendelea kuitenda kazi yake aliyotupa hapa Duniani.
DUNIANI KUNA MAKUNDI MENGI YA WATU LAKINI LEO HII NAOMBA NIKUPE AINA MBILI ZA WATU UNAOWEZA KUKUTANA NAO KWENYE MAISHA ili ujue na kuchagua aina ya mtu wa kuambatana naye kwa ajili ya hatima njema ya kesho yako na watu hawa wawili ni :-
1. MTUMWA WA LEO LAKINI KESHO YAKE IMEBEBA UFALME.
Huyu ni mtu anayeonekana yupo chini leo hii lakini ndani yake amebeba kesho iliyo juu yaani ni mtu mwenye dhiki na shida leo hii lakini kesho yake imejaa shibe na raha nyingi yaani uhalisia wa maisha yake umejaa shida nyingi kwa wakati huu lakini ndani yake amebeba kesho kubwa.
📌Hili ni kundi la watu mfano wa Daudi aliyekuwa mchunga kondoo maporini huko lakini kesho yake ilikuwa imebeba ufalme wa Taifa teule la Israeli yaani kwa sura ya nje na walioitazama leo ya Daudi walimuona shamba boy lakini kesho yake ilikuwa imebeba ukuu kuliko wote waliokuwa kwenye uongozi wa Israeli.
📌 Hili ni kundi la mfano wa YUSUFU mwana wa Yakobo aliyekuwa mfanyakazi ndani ya nyumba ya potifa, aliyekuwa mfungwa na mtumwa katika nchi ya Misri lakini kesho yake ilikuwa imeubeba uongozi mkubwa wa nchi ya Misri kama waziri Mkuu.
Walioitazama leo ya Yusufu walimuona kama houseboy aliyekosa makazi au mfungwa asiyekuwa na kesho ya maana lakini kesho yake ilikuwa imebeba hatima ya taifa zima la Misri na Israeli.
HILI NI KUNDI LINALOHITAJI MOYO MKUU KUAMBATANA NAO KWANI LEO YAO INAKUHITAJI WEWE UWASHIKE MKONO, UKIAMBATANA NAO HAWANA KITU KIKUBWA CHA KUKUPATIA LEO HII LAKINI KESHO ZAO ZIMEJAA UKUBWA.
Kwa sasa unaweza kuzikwepa simu zao ukaona wanakulilia shida lakini simu moja ya kesho yake inaweza kuwa na maana kubwa sana kwenye maisha yako. Usipokuwa rohoni ni rahisi kuwapuuza na unaweza kuwadharau hata kuwasahau kama mfungwa aliyemsahau Yusufu Gerezani lakini kesho akimuona waziri mkuu anaweza kutamani siku zirudi nyuma.
🖍️Huyu anaweza kuwa mtumishi wa Mungu mwenye huduma changa leo hii ambayo ukiitazama unamuona amekosa kazi lakini kesho yake imebeba huduma kubwa yenye mguso.
🖍️ Anaweza kuwa mwanaume anayekujia
Leo hii apate kukuoa lakini ukimtazama ukamuona hawezi kukufaa kwa sababu ya leo yake lakini ukikutana kwenye kesho yake unaweza kujiuliza ilikuwaje nikamkataa?
🖍️ Anaweza kuwa maskini wa leo anayeomba msaada na anayeonekana hana umuhimu lakini kesho yake imebeba msaada mkubwa utakaoutamani kuufikia.
WATU HAWA NI RAHISI SANA KUWAFIKIA KWENYE LEO ZAO KWANI WANAPATIKANA KIRAHISI LAKINI USIPOKUWA NA MAHUSIANAO NAO KWENYE LEO ZAO NI VIGUMU KUWAFIKIA KWENYE KESHO ZAO BILA CONNECTION.
Hawa ndio mtaa huwashangaa kwa kusema yule jamaa alikuwa machinga lakini sasa hivi ana makampuni, alikuwa maskini tu lakini sasa hivi hagusiki tena.
UNAHITAJI HEKIMA YA KIMUNGU KUISHI NA
KUNDI HILI KWANI UKIIKOSA HEKIMA HII UNAWEZA KUWAUMIZA WATU WALIOIBEBA HATIMA YAKO BORA YA KESHO.
Unahitaji kuishi kwa kumheshimu kila mtu kwa pasina kuitazama leo yake unayoiona kwani ipo kesho yake isiyoonekana ambayo imebeba ukubwa.
Mtu huyu anaweza kuwa mfanyakazi wako kama daudi nyumbani pa sauli lakini kesho ni mfalme na anaweza kuwa mdogo kama Yusufu lakini kesho yake ni waziri mkuu.
📌 USIWADHARAU WATU HAWA KWA LEO ZAO NDOGO ILA MSHUKURU MUNGU KWA KURUHUSU WAKUTANE NA WEWE ILI WAKUKUMBUKE KWENYE UKUBWA WAO KAMA YONATHANI ALIVYOLITAMBUA HILO KWA DAUDI.
Leo yao ni rahisi kuwapata lakini kesho yao huwezi kuwakaribia wala kuwagusa tena.
KATIKATI YA HAO WADOGO WAPO WENGI WAKUBWA WA KUKUSHIKA MKONO WAKIWA IKULU.
NENO LINASEMA:-
1 Samweli 2:6-8
[6]BWANA huua, naye hufanya kuwa hai;
Hushusha hata kuzimu, tena huleta juu.
[7]BWANA hufukarisha mtu, naye hutajirisha;
Hushusha chini, tena huinua juu.
[8]Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu;
Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA,
Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
Wakuu hawapatikani ikulu ila wakuu wanatoka mavumbini.
ASOMAYE NA AFAHAMU.
Facebook Msemaji Wa Injili