Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
KAMATI ya Rufaa ya chama cha upinzani nchini Kenya cha ODM imeahirisha mikutano yake hadi itakapotangazwa tena hapo baadae.
Willis Otieno, mwenyekiti wa kamati hiyo, aliahirisha vikao hivyo kwa muda usiojulikana, kutokana na wasiwasi wa usalama kwa wanachama wa kamati hiyo.
Hili limetokea baada ya kundi la watu waliovalia nguo nyeusi kuvamia mkutano wa kamati hiyo katika hoteli ya Marsh Park jijini Nairobi, ambapo kamati hiyo ilikuwa ikifanya mikutano yake, hivyo kuharibu maendeleo yake.
“Wote tuna wasiwasi juu ya usalama wa maisha yetu. Tunafanya kila linalowezekana kumaliza matatizo ambayo yalitokea wakati wa chaguzi za uteuzi kwa wagombea wa chama. Lakini tulivamiwa na ilibidi tuondolewe kupelekwa sehemu salama,” Otieno alisema.
Kamati hiyo imekuwa ikifanya kazi kushughulikia rufaa zilizopelekwa na wanachama wa chama hicho kufuatia chaguzi zilizokuwa na ushindani mkali ili kupata wagombea watakaokiwakilisha chama hicho katika uchaguzi mkuu. Chaguzi hizo za ndani zilifanyika kati ya tarehe 13 na 30 Aprili mwaka huu.
Watu hao walivamia kikao hicho na kuwapiga baadhi ya wanasiasa ambao waliitwa ili kusikiliza maamuzi ya kamati hiyo.
Ochieng Daima na Vincent Kodera, ambao walihudhuria kikao hicho, walipigwa pamoja na mwanasheria wao, Martin Onyango. Wagombea hao wawili wa Nyakach, Kaunti ya Kisumu, na walikuwa wakipinga ushindi wa Mbunge wa eneo hilo Aduma Awuor.
Shambulizi hilo liliwajeruhi wagombea hao pamoja na mwanasheria hao hadi kutokwa na damu katika maeneo ya pua na kinywani.
Chama cha ODM kimegubikwa na machafuko kwenye chaguzi hizo, kutokana na madai ya kuiba kura, na matokeo ya awali kufutwa na Bodi ya Uchaguzi ya Taifa ya chama hicho.
Chanzo: