Watu wasiojulikana

Sep 29, 2016
34
125
Ameandika Mohammed Ghassani

WATU WASOJULIKANA

Usiombe wakujuwe, watu wasojulikana
Wala wasikutambuwe, kwa sura wala kwa jina
Wawe mbalimbali nawe, kwa usiku na mchana
Sababu wakikujuwa
Watakuja kuchukuwa
Kipoloni wakutie
Chatu wakamrushie
Nyamunyamu akakule
Nyafunyafu akumeze
Hao watu wasojulikana!

Kisha tutatangaziwa, watu wasojulikana
Ndio waliokutwaa, kwenda pasojulikana
Uchunguzi waendelea, kwa lisilojulikana
Kisha jalada la kesi
Lipotee kama moshi
Liyeyuke
Litoweke
Lende kusojulikana!

Mohammed K. Ghassani,
16 Disemba 2016
Bonn
 

General Mangi

JF-Expert Member
Dec 21, 2013
14,796
2,000
Bara la Afrika haliishi giza
Rangi za watu hadi mioyo yao ina giza.
Sisi Africa tuneharibiwa na utamaduni wa kizungu.
Tulipaswa kuishi yale maisha yetu ya kuwasha moto kwa kijiti, kutembea uchi na kutambikia.

Haya maisha tuliyoletewa yanatugharimu sanaa.
Ndio maana tunaonekana wa ajabu ajabu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom