Watu waikimbia jiji la Nairobi

Watu waikimbia jiji la Nairobi

Imeloa

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2013
Posts
17,999
Reaction score
21,560
Kufuatia hofu ya kuzuka kwa vurugu baada ya zoezi la upigaji kura kumalizika siku ya jumanne 08/08/2017, wimbi la watu kuanza kuukimbia jiji la Nairobi limeanza kushuhudiwa.

Sambamba na hilo, watu wanaonekana wakimiminika kwenye maduka mbalimbali makubwa kujipatia mahitaji muhimu kama Unga, Mchele, Mafuta ya kupikia, Sabuni, Maziwa, Dawa nk itakayoweza kuwasukuma kwa wiki moja hadi mbili kuhofia uwezekano wa kuzuka kwa ghasia hasa baada ya matokeo kutangazwa.

Kuna taarifa zimeenea nchini Kenya kuwa serikali ya chama kinachotawala cha Jubilee kimeandaa mkakati wa kuchakachua matokeo ili kubaki madarakani.

Tayari watu wanakihusisha kifo cha aliyekuwa meneja wa kitengo cha mawasiliano cha tume ya uchaguzi IEBC Bw. Chris Msando na njama hizo za kuiba kura, kwani wanadai Bw. Msando kabla hajauliwa alilazimishwa na wauaji wake kusalimisha password na mbinu alizokuwa akitumia kulindia mfumo maalum wa computer inayotumika ktk kupokea na kutunza matokeo.

Hivyo basi pamoja na msimamo wa muungano wa upinzani Nasa kwamba katu hawatakubali kuibiwa kura, watu wengi wanatafsiri hali ya mambo kuwa inaweza isiwe nzuri kufuatia "Stakes" ambazo zinahusishwa na uchaguzi huu kwa pande zote.

Pia kitendo cha serikali kuvamia ofisi ya ushirika wa upinzani Nasa kwa madai ya kutaka kuzuia wapinzani wasiweze kujumlisha matokeo ya uchaguzi ni kitendo kinachozidi kuchochea hofu miongoni mwa wananchi wengi japo Nasa wamedai wana vituo vingi vya kujumlishia matokeo nchini Kenya.

Vyovyote itakavyokuwa, uchaguzi huo unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute ambapo mshindi inatarajiwa atapatikana kwa kura ya hatua ya kwanza, yani haitarajiwi kuwa na marudio ya kura kwa wawili watakaokua wametangulia (Run-Off) na matokeo yote kwa masanduku sita ikiwemo ya urais, yatatangazwa moja kwa moja vituoni na tume ya uchaguzi itatangaza mshindi wa urais tu.
 
Amani itawale itawale throughout

Sent from my Priceless H40-D00 using JamiiForums mobile app
 
Siasa za Afrika zimejaa maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma
 
Ukishajua siasa za kenya zimejengwa kikabila . It's simple to predict the victory.
 
Back
Top Bottom