Watu wa Kanda ya Ziwa tulidanganywa na rais wa awamu ya nne

koryo

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
639
278
Kama mnavyofahamu Rais wa awamu ya nne alituahidi kwenye kampeni zake kuwa ataleta MELI KUBWA ya kisasa katika Ziwa Victoria na hivyo tukampa kura za kishindo.

Meli zote zilizopo sasa hivi katika Ziwa Victoria siyo salama na ieleweke usafiri wa uhakika na wenye bei nafuu ni wa kutumia vyombo vya usafiri vya majini.

Mazao mengi kwa matumiizi ya binadamu kama ndizi,mihogo, maharage, samaki nk.yanasafirishwa kutoka Bukoba kuja Mwanza kwa meli na kwa gharama nafuu kabisa.

Hivi sasa hakuna huduma ya meli kutokana na meli kuharibika. Kabla ya kumaliza muda wake angetuetuomba MSAMAHA kwa kutudanganya na hivyo tukamsamehe kwa kutoleta meli mpya.

Namfahamu Mhe. wa HAPA KAZI TU haitafika Desemba, 2017 kabla hatujapata meli mpya.
 
ni miaka mingi tu sasa watu wa kanda ya ziwa tumetumika kama mtaji wa ccm kuelekea ikulu tunadanganywa kama watoto na hatujitambui huyu naye kaahidi daraja la kigongo ferry - busisi na tunashangilia kama mazuzu ili hali ni ndoto za mchana kutimiza hilo
 
Watu wa Kanda ya Ziwa hasa wana CCM walivunja rekodi ya Dunia kwa kuandamana na kumuunga mkono Kikwete kuwa wao hawali mapanki! Na baada ya siku tatu BBC wakathibitisha kuwa Mapanki yanaliwa sana na kila aliye hojiwa alikiri kuwahi kula au ana wafahamu watu wanao kula mapanki. Na kwakua JK ni muungwana akakiri kukosea.
 
Back
Top Bottom