Watu saba wanashikiliwa na Polisi Mara kwa tuhuma za kubaka na kunyonga

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,563
21,665
Jeshi la Polisi mkoani Mara linawashikilia watu saba kwa tuhuma za kumbaka kisha kunyongwa hadi kufa mtoto wa kike mwenye umri wa miaka minne na nusu Mariam Deaogratus ambaye aliyekuwa mwanafunzi wa shule ya awali ya makoko katika manispaa ya Musoma.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mara kamishna msaidizi wa jeshi la polisi ACP Philip Alex Kalangi, amesema watu hao wamekamatwa siku moja tu baada ya kutokea kwa tukio hilo la kikatili.

Awali kamanda alisema mtoto huyo alikumbwa na mkasa huo muda mfupi baada ya kuondoka nyumbani kwao jioni ya Februari 23 mwaka huu kwenda shule kwa ajili ya masoma ya ziada, lakini akuonekana tena hadi saa 2 usiku wa siku hiyo Februari 23, mwili wake ulipokutwa ametupwa katika nyumba ambayo ujenzi wake unaendelea.

Akizungumzia tukio hilo mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Musoma, kamishina mwandamizi mstaafu wa jeshi la polisi Zeloth Stephen, amesema vyombo vya dola vitafanya kila Nnjia katika kuhakikisha mtu yoyote ambaye amefanya kitendo hicho cha kikatili anakamatwa na kufikishwa mara moja katika vyombo vya sheria.
 
Tunaomba jeshi letu litumie DNA mara zote kwenye matukio kama haya sababu hawatakana kama DNA ipo.
 
Tunaomba jeshi letu litumie DNA mara zote kwenye matukio kama haya sababu hawatakana kama DNA ipo.


pamoja na teknolojia kusaidia ktk kupata ushahidi, lkn jeshi la tz ni nadra sn kutumia teknoloja ya fingerprint na DNA ktk ushahidi wao.

hawana tofauti na mpiga ramli....
 
Jamani jamani, nahisi kuna Vitu tunafanya hadi shetani mwenyewe anatushangaa. Mtoto wa miaka minne akabakwe na mijitu mizima ilokomaa, ni genye za aina gani hizo au ndo mambo ya kishirikina? Eeeh Mungu tuhurumie tu
 
Back
Top Bottom