Watu pori - Nilie na nani

Watu pori - Nilie na nani

NGAYANIMO

Member
Joined
Feb 17, 2026
Posts
36
Reaction score
55
WATU PORI " AFANDE SELE & MC KOBA" NELIE NA NANI

Intro: Afande sele
Mh..!!
Aah.!!
Mapenzi
Hahahaha
Ooh..! Labda haikuwa Bahati Yangu
Bwana Haya
Aah..!
Sawa

Chorus: MC koba

Mwezenu nalia
Nilie na Nani..?
"Ooh..!! Nalia Mimi
Nilie na Nani.?
Sikupenda Mimi
Kasababisha shetani
Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani..?

Mwezenu nalia
Nilie na Nani..?
"Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani.?
Sikupenda Mimi
Kasababisha shetani
Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani..?

Eeeh..!!"

Verse 1. "Afande sele"

Maana akumbuki mara ya Kwanza nilipo Kukutana Nae/
Nilimpenda nikapanga Kufa Nae/
Kila dalili nilionyesha na kisha Kumueleza nataka kuishi Nae/
Tupange mikakati maisha Yetu ya Baadae/
Yaani Tuishi wawili mke na mume na Tuzae/
Mchumba akajibu Amna Noma..!!
Ila ningoje akisha Soma, Akimaliza Masomo/
Ndo Kwanza Yupo kidato cha Kwanza/
Lakini Mimi sikujali,Nikamsubiri/
Kidato cha pili fika mpaka cha Tatu/
Na Gharamia Soda, chips..!!
Mwisho ka pass kaenda Mpaka form six (6)/
Aah..!!
Nikazindi kummiss
Alipopata Boss kwenda Ulaya/
Me nikidhani hakuna Ubaya/
Nikizingatia eeeh.!!
Akisharudi tutajenga familia/
Kumbe pata potea/
Naliishia kunawa Mzungu akananilia/
Eeeh..!
Iseehe..!!

Chorus: MC koba

Mwezenu nalia
Nilie na Nani..?
"Ooh..!! Nalia Mimi
Nilie na Nani.?
Sikupenda Mimi
Kasababisha shetani
Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani..?

Mwezenu nalia
Nilie na Nani..?
"Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani.?
Sikupenda Mimi
Kasababisha shetani
Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani..?

"
Verse 2. "MC" Koba

Nashindwa Kuelewa shetani kiumbe wa aina Gani/
Maana mabaya yote analeta Yenye Duniani/
Tazameni jamani..!!, mwezenu nilipo naachwa mpweke nyikani/
Dawa ya kiu ni maji kwenda kinywani/
Ila wa moyo wangu mpenzi wangu haonekani/
Sasa sijui mwezenu nitaponywa na kitu Gani/
kwa vile kama mapenzi majani pita shingo/
Mimi ni kijana mdogo bado na haki ya kupenda/
Tatizo ni upofu machoni mwangu umetanda/
Sioni ni mpende Nani..? Ambae atonitenda kama Yule wa zamani/
Kifupi nipo ngizani na bado nalia/
Sielewi nilie na Nani..?..
Eeeh.!!

Chorus: "MC" KOBA

"Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani..?
Mwezenu nalia
Ooh.!!
Nilie na Nani..?
Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani..?
Sikupenda Mimi
Kasababisha shetani
Ooh..!! Nalia
Nilie na Nani..?
Eeeh..!!"

Verse.3 "Afande sele"

Mchumba anitaki/
Tena..!!
Hataki hata kuniona/
Na nikipiga simu akipokea ananitukana/
Balaa sina Raha, sina Furaha/
Najiona kama fala/
Bora ningempa Mimba kabla hajakwenda Ulaya/
Mapenzi kitu kibaya/
Zaidi..!!
Kukataliwa ndo mbaya/
Unaweza kukonda ukazushiwa unamiwaya/
Mawazo..!!
Mawazo..!!
Eeeh..!!
Nikikumbuka Penzi letu pale Mwanzo/
Naona kama Ingizo/
Sometime ni mafunzo/
Kwa vile sasa nimeAmini/
Kweli mapenzi hayana mthamini/
Nilipopata Salamu zake sikuamini/
Kama engenikana Angeniona Sina Maana/
Kwa jinsi, Tulivyopendana/
Nimechanganyikiwa najiona kama mkiwa/
Sitamani kula/
Sitamani kulala/
Na mawazo yanazindi
Rafiki zake wakinionyesha zawadi na Card/
Za harusi yake itakayo fungwa akisharudi/
Na mume Wake Zungu/
Japo..! Na machungu
Sina cha kusema .!. ,Cha zaidi namuomba Mungu/
Tu.!
Anibariki, Ambariki
Hata kama tumeachana/
Sio vyema Kuishi kwa chuki/
Kwani mapenzi yanapita Maisha yanaendelea/
Hakuna anaejua Baada ya Muda mfupi Ni kipi..? kitamtokea Maishani/
Japo..! Unipendi Moyoni/
Jaribu kunificha usinionyeshe Machoni/
Bragwiii..

End..

Ukwaju wa kitambo nilipata Fursa ya kuzungumza na Selemani Msindi a.k.a Afande sele kuhusu wimbo Huu "Nilie na Nani" wimbo unaopatikana Katika Album Ya Crew " Watu PORI" ambapo ni afande sele,Lameck ditto ( Dogo Ditto) na MC Koba.... Album inajulikana kwa jina la " Nafsi ya Mtu" na haya ni aliyoyanena.

"Wimbo wa nilie na Nani..? Nilifanya na "MC" KOBA upo Katika Album ya "watu PORI" inaitwa " nafsi ya Mtu" ila huu wimbo nilifanya na "MC" KOBA Tu Wimbo huu wa "nilie na Nani" Asili ya wimbo Huu sio kwamba maybe Mimi nilitokewa na Jambo Hilo "Hapana" .
Nafahamu kuwa ni aina ya story ambayo imekwisha watokea watu wengi...

Sababu kabisa ya Mimi kuwa na idea ya wimbo Huu...
Mimi binafsi naweza kusema imetokana Na nyimbo ya zamani , Maana Mimi kiukweli Toka zamani ni mpenzi wa nyimbo za zamani, nyimbo za zamani za makundi mbalimbali ya Dansi kama Vile..
DCC Mlimani Park Orchestra (au Mlimani Park), ottu jazz nk.

Napenda Sana nyimbo zao. Kwa hiyo wimbo Huu " Nilie na Nani" nilitaka kufanya na Mzee " Hassan Rehani Bitchuka" Member wa Kundi la Muziki wa Dansi "DCC Mlimani Park Orchestra" " Sikinde Ngoma Ukae"

kupitia wimbo wa "Sikinde Ngoma Ukae" kwenye wimbo wao unaitwa " sikufikiria" nyimbo hii ina mkasa huo huo kama nilivyoimba Mimi Katika wimbo "Nilie na Nani" na MC Koba.Story Katika wimbo huo wa Mzee Bichuka unasema:

"Mchumba wake alikwenda Ulaya lakini hakurudi "

Kutokana na Utunzi kubadirika Katika Muziki Aina ya Rap / Hip hop Enzi Hizo Mimi Afande sele Nilitaka kutumia chorus hiyo ya Mzee Bitchuka " kwa kutumia original Chorus vision" ya nyimbo la kundi lake la "sikinde Ngoma Ukae" wimbo unaoitwa "sikufikiria" ila Mimi nijaribu kuielezea hiyo story angalau iwe kwa urefu kwa mfumo wa Kurap .

Maana Hadithi au mikasa mara nyingi kwenye nyimbo za Band hawaimbi kwa urefu simulizi Hizo, ila Mimi nikaona kwenye Muziki wa Hip hop Jambo Hilo naweza kuelezea Mkasa huo kwa Urefu zaidi , ILi kwa yoyote yule atakae weza kupata chance ya kusikia kisa hicho aweze kuguswa Katika kizazi ama Generation hii ya Hip hop , nilitamani Sana kutumia Chorus ya Mzee Bitchuka ila Taratibu za Band Yake Enzi Hizo "sikinde Ngoma Ukae" zilipelekea kushinda kumpata"

Na Mimi Enzi Hizo huko mjini morogoro nilikuwa Tayari nina Crew ya "watu PORI" Mimi ,"MC" KOBA & Dogo Ditto ( Lameck ditto) nikaona pia ni njia ya kuwapa Fursa Vijana Wangu maana pia Nia Yangu kubwa ilikuwa ni kuwakuza Kimuziki Vijana hao ..

Ndio alipowapa chance ya kuimba "MC" KOBA alifiti zaidi kuliko Dogo Ditto na Mimi nikampa nafasi ya kuimba chorus hiyo.

Maana hata ukiisikiliza kwa makini utagundua ina karibiana kabisa na style ya uimbaji wa kundi la " Daz nundaZ" Maana mimi Enzi Hizo nilikuwa karibu sana na kundi la Daz nundaZ " hasa kwa hawa wasanii wawili " Daz Baba Na ferooz" ..

Kwanza before kurekodiwa nilitaka kufanya na "Daz Baba" nilipompa chance "MC" KOBA nafasi Nae alipita mule mule kama style ya uimbaji WA wasanii kutoka Crew Ya Daz nundaZ hasa wasanii wawili " Daz Baba Na ferooz " ila kama nilivyokueleza Asili ya wimbo Huu uliofanyika Katika Studio za DJ bonnie luv " "Nawingu Studio" wakati huo pale studio "Nawingu Studio" Alikuwepo Producer na Msanii mmoja anaitwa ," Juma" lakini baadae alijiita "Cheche" alifanya Ile Video ( shooting) Ya wimbo wa Baba unaitwa " Zoba" nadhani kwa sasa Yupo pale " Azam" anafanya kazi ya ku translate/ kutafisiri Zile cinema na Tamthilia..

, lakini kiasili Yule ni Producer na walikuwa na Crew Yao Enzi Hizo inaitwa "Neck Breakerz" baada ya kundi Hilo Kufa ndio akaamua kwenda kwa DJ bonnie luv pale "Nawingu Studio" na kuamua kuwa producer na ndio nakamkuta kwa wakati huo pale " Studio" ndio nikafanya wimbo huo na Yenye " Nilie na Nani"

Studio ilikuwa ni ya DJ bonnie luv ila kuanzia kutengeneza Beat / instrumental,kuweka Vocal NK tulifanya na Huyo Brother anaitwa " Juma" a.k.a manywele Mengi...

"Nilie na Nani featuring MC KOBA upo Katika Album inaitwa " Nafsi ya Mtu" Album yangu Ya Tatu nadhani Baada ya "Mkuki Moyoni" nikaja na "Darubini Kali" baadae ndio nikaja na hiyo Album inaitwa " Nafsi ya Mtu" ndio nikaja na Album yangu Ya nne ilikuwa inaitwa " karata Dume"Baadae nikaja na Album yangu Ya Tano inaitwa " king dom" ambayo ndio ilikuwa ni Album yangu Ya mwisho Enzi Hizo wakati wa hutoaji wa Album Hapa Bongo .

Kwa hiyo wimbo wa "Nilie na Nani" ni project za Mwanzo kabisa Baada ya Crew ya " Ghetto boys kuvunjika wasanii waliounda kundi la ghetto boys Enzi Hizo ni Afande sele,kasa boy, juma mjivuni,mdogo Ditto, bwana samu,Mc koba na Baadae Akaongezeka Msanii Ballet.

Baadhi ya nyimbo zilizoimbwa na Crew ya Ghetto boys ni
Sikufichi, hatuna Ajila ft. Afande sele na Yote Bure ft. Professor jay

kuvunjika kwa Ghetto boy's na kuanzishwa kwa " Watu PORI " ndio tukaanza Rasmi kama Crew ya watu PORI na Album ya " Nafsi ya Mtu " Yenye nyimbo kama vile . Usinichukie, Nyumba za kupaga, Nafsi ya Mtu Yenyewe na nyimbo nyingine kadhaa takiribani nyimbo 12 jumla na hiyo " Nilie na Nani" Ndani yake.

Idea ya wimbo huo wa " Nilie na Nani," kama nilivyokueleza sio kwamba Mimi nilikuja na idea moja kwa moja angali nilikuwa nafahamu Vituko kama hivyo kwamba kuna watu wanasomesha wasichana,wanasimamia kila kitu ila kwa Bahati mbaya mahusiono
Yao huko mbele yanakuja kuvunjika.

Kama alivyoimba nyalimkela " Stera" kwamba mchumba wake alikwenda japani " Kusoma" jamaa akauza kila kitu kwaajili ya Gharama za Elimu ya juu huko Japan ila cha Ajabu Yule mwanamke aliporudi kutoka Japani Baada ya kuhitumu Elimu ya majuu huko Japani alirudi na mjapani .

Wimbo huo Huu ,"Nilie na Nani" umetokana na Idea ya wimbo wa Band inaitwa "Sikinde Ngoma Ukae" unaitwa " sikufikiria ambao uliimba na utunzi WA Mzee Hassan rehani Bitchuka"..

Bitchuka alipata umaarufu na kupendwa na halaiki ya wapenzi wa muziki wa dansi katika nchi mbalimbali za Afrika ya Mashariki na Kati. Katika miaka hasa ya 80, redio za mataifa ya nje, licha ya za napa nchini, zilizicheza sana nyimbo za DDC Mlimani Park na Juwata Jazz zilizoimbwa na Bitchuka.

Baadhi ya nyimbo alizoimba, nyingi katika hizo ametunga mwenyewe ni kama; (NUTA) Halima, Kilimo cha kufa na kupona, (JUWATA) Nidhamu ya kazi, Mwana acha wizi, Mpenzi Zarina (aliomtungia mkewe), Sogea karibu, Uzuri si shani, Selemani, Mariamu ninakujibu, (Mlimani Park)..

Tufanye kazi kwa nidhamu, Duniani kuna mambo, Tucheze Sikinde, Tende Halua, Penzi la fukara, Kupenda sio ndoto, Aija, Hiba, Hasira, Talaka ya hasira, Nawashukuru wazazi, Penzi la mwisho, Fikirini nisamehe, Asiyesikia la wazazi, Shemeji Issa, Mume wangu Jerry, Mv. Mapenzi I, Uhuru wa Zimbabwe, na nyingine nyingi.

top fans
Ukwaju wa kitambo
0767542202
1771511974794.jpg
1771511445987.jpg
Bitchuka_2015.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom