Watu ni sehemu ya maendeleo

Watu ni sehemu ya maendeleo

Joined
Oct 5, 2018
Posts
33
Reaction score
58
Kati ya vitu vinne alivyovisema mwalimu Nyerere ili TAIFA liendelee ni WATU. Ukitoa uongozi bora, ardhi na siasa safi. Tatizo ni kwamba watu hawajioni tena sehemu muhimu katika kuliendeleza TAIFA lao, najua anguko la uzalendo ni sababu kuu.

Fikiria hili; angalau 60% yetu tumepita katika taasisi mbalimbali za elimu kama vile shule. Tukisema kila mmoja aliyepita kwenye shule fulani awe na taratibu ya kuchangia maendeleo ya shule aliyopita unadhani shule zitakuwa na vyoo au majengo yaliyochakaa kiasi cha kutisha au kutofaa cha kabisa?

NB: Pichani ni picha ya choo ya shule moja mkoani Iringa iliyofungwa kutokana na ubovu wa vyoo.

~ Justine Kakoko

IMG_20200306_084406.jpg
 
Hii mambo ya Nyerere Nyerere inapotezea watu muda bana kafanya yake ameenda muacheni apumzike sio tunaishi kungangania fikra za mtu wa miaka iyo hata kupiga rangi unaenda kusomea akati sa hv unaingia youtube tuu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio lazima watu muendelee kuishi kwa fikra za late Nyerere ...kwani Nyerere alikuwa ndo anaonekana Hana Akili nyingi kuwazid watanzania wote.
Toa shida ya hiyo fikra ya Nyerere ili hoja yako isomeke kiweledi. Ukitoa hoja kama hivyo hautojitofautisha na kichaa.
 
hii mambo ya nyerere nyerere inapotezea watu muda bana kafanya yake ameenda muacheni apumzike sio tunaishi kungangania fikra za mtu wa miaka iyo hata kupiga rangi unaenda kusomea akati sa hv unaingia youtube tuu aisee

Sent using Jamii Forums mobile app
Kataa hoja kwa hoja ili usionekane unayakataa mambo kwa chuki binafsi. Kuna mambo huwa yanapitwa na wakati, lakini kuna mambo huwa yanabakia kuwa relevant. Mawazo mengi ya Nyerere yamepitwa na wakati, lakini yanayoishi tusiache kuendelea kuyafufua.
 
Uzalendo maana iliyo rasmi ni ile hali ya mtu kuipenda, kuithamini na kujitoa kwa ajili ya nchi yake kwa msingi wa kitabia, utamaduni, siasa au historia inakaribiana sana na utaifa.

Kwa maana hiyo, mtu kujitoa kwa ajili ya taasisi fulani iliyowahi kumjenga au kumsaidia bado ni uzalendo. Labda kama uamue kuja na maana mpya. Mtu kuja na maana mpya kwenye tabaka la watu wanaofikiri ni jambo la kawaida kabisa.
 
Sio bora watu Bali watu wenye maarifa na nguvu na afya . Wale wanaoweza kushiriki katika nyanja za uzalishaji. Jamii ikiwa na watoto na wezee tegemezi hesabu hasara hapo hakuna maendeleo. Jamii zenye iliterate and sick population haiwezi kuwanyenzo ya uchumi Bali ni liability population.

Msingi huo ndo unaofanya jamii zetu kuwa duni na kukosa maendeleo. Tuna kundi kubwa la tegemezi ( watoto, wazee, wagonjwa na vijana wasio na ujuzi)

Ndiyo maana mwalimu alisema watu sio maana ya watu bali rasilimali watu. Najua fika elimu yetu haituandai kuwa wenye uwezo wa kujitegemea, hata vijana wengi bado ni tegemezi. Lakini, kwa kuwa tuna watu tegemezi, tunapaswa kukaa kimya na tusikumbushane umuhimu wa watu kuweza kujitegemea na kuyaendeleza mataifa yao.?
 
Watu ndiyo maendeleo yenyewe na siyo sehemu ya hayo maendeleo tu.Kuwatenga watu na maendeleo kama sehemu mbili tofauti ni hatari sana.
Watu na maendeleo ni sehemu ileile moja katika namna tofauti.
Kujali watu nikujali maendeleo na kujali maendeleo ni kujali watu.
 
Uisome post vizuri. Vitu vinne vyote ni sehemu muhimu ya maendeleo. Hauwezi kuendelea kama hauna ardhi. Afrika Kusini kuna watu wenye nguvu na uwezo lakini hawana ardhi. Maendeleo yanakujaje bila ardhi? Au siasa chafu kama ya Tanzania maendeleo yatakujaje? Leo nimeongelea tu watu, lakini vinne vyote ni muhimu.
 
Mimi nalipa kodi ujenzi wa shule ni jukumu la ninaemlipa kodi hapo iringa Huyo bwana afya wa wilaya ilipo shule ni wakufuta kazi {jipu}

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom