kinganola
Senior Member
- Aug 16, 2011
- 117
- 30
Ni siku chache tu zimepita Tangu wana kijiji wa Endamana wilayani Manyara walipo amua kutembeza msako wa boma kwa boma kukamata wapika Gongo,zoezi lilifanikiwa lakini chakusikitisha,jamaa wameamua kulipiza kisasi na kumuua kiongozi za zoezi hilo,Wana nchi wamekuja juu tena na kuchoma moto nyumba za watu wanao watuhumu kuwa ndo wauwaji.Sasa mi najiuliza,Kazi ya polisi ni nini,mpaka wananchi wana amua kusaka wapika Gongo,ni kwamba Polisi imeshindwa kazi.Mbaya zaidi walipo wakamata watuhumiwa,wakawatoza faini ya ng'ombe na Polisi ikaliona hili,sasa wameuana ndo mnakwenda,mnakwenda kufanya nini?