Watu bwana

Dengue

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Posts
2,050
Reaction score
1,469
Kila mji unaokwenda hawakosi cha kukuagiza. Kama waenda Mbeya utasikia, "Tuletee maparachichi na mchele." Ukienda Moshi unaagizwa, "Usisahau kutuletea kahawa." Uendapo Dodoma utasikia, "Utuletee zabibu na karanga." Ukienda Tabora wapo tu, "Pliiiiz utununulie asali huko." Ukienda Morogoro wanaagiza, "Tuletee magimbi basi." Kama waenda Bagamoyo waagizwa, "Mananasi ya kule matamu usisahau kutuletea." Unapokwenda Tanga utasikia, "Tuletee machungwa jamani!" Kama ni safari ya Songea, "Usisahau viazi vya Songea." Unapokwenda Mtwara unaagizwa, "Tuletee korosho unaporudi." Unapokwenda Kigoma, "Jamani rudi na mafuta ya mawese na migebuka." Ukisema safari inaishia Singida wana wewe tu, "Basi utuletee mafuta ya alizeti." Ukiwaambia unakwenda Mwanza wanaagiza, "Utuletee samaki sana sana Sato." Kama waenda Bukoba hawachoki tu, "Tafadhali utuletee senene!" Kasheshe sasa kama safari yako inaishia Iringa. Utasikia sasa, "Niletee mdada wa kazi jamani!
 
Endeleza mikoa mingine.
 
Kwahiyo Iringa wanalima wasichana wakazi! ww mbona unawashushia hadhi wahehe! wasije wakaSadaam Hussein bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…