Shirika la kibinaadamu la Human Rights
Watch linasema kuwa vikosi vya usalama
ini DR Congo vimewaua takriban watu 34
wakati wa maandamano wiki hii.
Mazungumzo yanayoendeshwa na kanisa
katoliki yanaendelea mjini Kinshasa ,ili
kujaribu kumaliza mgogoro katika ya
upinzani na rais Joseph Kabila ambaye
alikataa kuondoka madarakani wakati
muda wake ulipokamilika siku ya
Jumatatu.
Kuna ripoti tofauti kwamba watu wengine
17 wameuawa kaskazini magharibi mwa
Congo.
Maafisa wa polisi wanadaiwa kukabiliana
na wanachama wa kundi moja la
madhehebu linaloamini kwamba mwisho
wa utawala wa Kabila ndio mwanzo wa
mwisho wa dunia.
Wakati huohuo Mamlaka nchini DRCongo
imewakamata watu kadhaa katika mji wa
pili kwa ukubwa nchini humo,
Lubumbashi.
Meya wa mji huo anasema kwamba
wanajeshi walikuwa wakiwakamata
wahalifu, japo wenyeji wa mji huo
wanasema waliokamatwa ni vijana
wanaoshukiwa kupinga utawala wa rais
Joseph Kabila.
HATUTAKI MAANDAMANO YOYOTE NCHINI KWETU.
Chanzo: BBC