Watu 18 wauawa katika mapigano mapya Somalia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Watu 18 wauawa katika mapigano mapya Somalia

Discussion in 'International Forum' started by bakuza, Apr 3, 2012.

 1. bakuza

  bakuza JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2012
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 488
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Watu 18 wauawa katika mapigano mapya Somalia [​IMG]Watu 18 wameawa na wengine kadhaa kujeruhiwa katika mapigano mapya yaliyotokea kusini magharibi mwa Somalia.
  Mwandishi wa Radio Tehran ameripoti kuwa, mapigano yaliyotokea kati ya wanamgambo wa ash Shabab na wanajeshi wa Somalia na Kenya yamepelekea kuuawa watu 18 na wengine kadhaa kujeruhiwa katika eneo la mpakani la Gedo la kusini magharibi mwa Somalia.
  Habari hizo zinaongeza kuwa, ndege za kivita za Kenya zikisaidiana na wanajeshi wengine wa nchi hiyo, zinaendelea kushambulia maeneo ya katikati mwa mji huo.
  Mmoja wa wakazi wa mji wa Gedo amesema kuwa, mashambulio hayo ya ndege za kivita za Kenya yamewalazimisha wanamgambo wa ash Shabab kurudi nyuma na kukimbilia kwenye vijiji vya pambizoni mwa mji huo.
  Watu walioshuhudia wamesema kuwa, wengi wa waliouawa katika mapigano hayo ni wanamgambo wa ash Shabab.
   
Loading...