beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,881
- 6,378
Watu wapatao 13 wameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa ikiwemo afisa wa polisi hapo Ijumaa katika shambulio la risasi kwenye jengo la serikali mjini Virginia Beach, Marekani.
Mkuu wa polisi Kames Cervera amesema mshambuliaji, ambaye alikuwa mfanyakazi wa jengo la manispaa, pia ameuawa.
Shambulio hilo limetokea saa kumi jioni baada ya mshambuliaji aliyekuwa na silaha kuingia katika jengo hilo na kuanza kufyatua risasi. Watu wanne waliopata majeraha wamefikishwa hospitali karibu na eneo hilo.
Mtu mmoja aliuliwa akiwa ndani ya gari lake, wakati wengine walikutikana katika ghorofa zote tatu za jengo hilo.
"Kutokana na milio ya risasi, maafisa wa polisi wanne waliweza kujua mshambuliaji alikuwa ghorofa gani ya jengo alipokuwa akiendeleza mashambulizi. Haraka walianza kumshambulia, na naweza kusema yalikuwa ni mapambano ya muda mrefu," amesema Cervera.
"Wakati wa makabiliano hayo ya risasi, maafisa wa polisi walifanikiwa kumzuia mshambuliaji kuendeleza mauaji zaidi ndani ya jengo."
Sababu ya shambulizi haijulikani
Maafisa wa polisi hawakutaja jina la mshambuliaji huyo, na nia yake bado haitambuliki, lakini wamesema alikuwa mfanyakazi wa muda mrefu katika jengo hilo, na aliuawa wakati wa makabiliano na polisi.
Miongoni mwa waliojeruhiwa ni afisa mmoja wa polisi, ambaye alinusurika kwa kuvaa vesti ya kuzuia risasi. Wote waliopata majeraha walikuwa wakifanyiwa upasuaji hospitali Ijumaa usiku.
Jengo hilo lilioko katika mji wa Virginia Beach -- mji wenye idadi ya watu wapatao 450,000 kilomita 320 kusini mashariki mwa Washington -- kawaida huwa na watu wapatao 400 wanaofanya kazi katika ofisi tofauti.
"Huu ni mkasa wa kusikitisha zaidi mjini Virginia Beach," amesema Meya Bobby Dyer akizungumza na waandishi habari. "Watu walioathirika na mkasa huu ni marafiki zetu, wafanyakazi wenzetu na majirani zetu."
Rais Donald Trump amearifiwa kuhusu shambulizi hilo na ikulu imesema anafuatilia kwa karibu.
Kulingana na kundi la kufuatilia mashambulizi ya bunduki nchini humo, hili ni shambulio la 150 mwaka huu la kuua watu wengi kwa kutumia risasi.