Watoto Wilayani Moshi wanajisiwa kwa kipindi cha mwaka mmoja

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Watoto wanne wa kike wenye umri wa miaka nane, wamebainika kubakwa na kunajisiwa kwa karibu mwaka mzima huku vijana wawili wanaowafanyia vitendo hivyo wakiwalipa Sh 500 kila mmoja.

Habari zinasema watoto hao wanaosoma darasa la tatu katika shule ya msingi ya Msaranga katika Manispaa ya Moshi, wamekuwa wakienda kufanyiwa vitendo asubuhi kabla ya kuingia darasani.

Uchunguzi wa madaktari wa hospitali ya rufaa ya mkoa Kilimanjaro ya Mawenzi umethibitisha watoto hao kuingiliwa sehemu za siri na kunajisiwa na pia wameambukizwa magonjwa ya zinaa.

Watoto hao wamekuwa wakifanyiwa vitendo hivyo kati ya saa 12:30 na saa 1:30 asubuhi na baadae hutakiwa kurudi saa 4:00 wakati wa mapumziko ili kuchukua Sh500 kama malipo ya kazi hiyo.

Tukio hilo ambalo limeibua hasira za wananchi, linafanana kwa kiasi na lile la mwanamuziki Nguza Viking “Babu Seya” na mwanae Jonson Nguza “Papii Kocha” wanaotumikia kifungo cha maisha jela.

Wanamuziki hao raia wa Congo walihukumiwa kifungo hicho mwaka 2004 kwa tuhuma za kubaka na kunajisi watoto 10 wenye umri wa miaka 6 na 8 wa shule ya msingi Mashujaa ya Jijini Dar Es Salaam.

Mzee Alex Massawe (sio jina lake halisi), mkazi wa Msaranga mjini Moshi, alisema kuwa Jumatano iliyopita, alishuku mwenendo usio wa kawaida wa mjukuu wake mwenye umri wa miaka nane.

Habari hii imeandikwa na gazeti la Mwananchi
 
Mtoto huyo alipoulizwa, alieleza maelezo yanayofanana na ya babu yake na kuwataja kwa majina vijana hao, mmoja jina lake likianzia na herufi J na mwingine jina lake likianzia na herufi W.

Kwanini wasiwe chini ya ulinzi mpaka habari hii inafika hapa, na kwanini majina yanafichwa kwa watu wenye unyama kama huo?
 
Hivi kwanini Majambazi wanatajwa majina haraka,ila watu wenye unyama huu hawatajwi majina.
Ta tatizo la sheria zetu zilivyo mbovu,utakuta unaambiwa kwamba hakuna ushahidi,mpaka waone MANIII ya mwanaume ndio uwe ushahidi,la sivyo utakuta anaachiwa.
 
Duuu hatar sana ....hawa wanaofanya hv vtendo ndo wapelekea kuongezeka kwa idadi ya masho* inafikia kipnd watoto wanazoea hvo v mchezo.........moshi wanakuja juu na hvo vtabia na tayar wanao shemej yao mzungu alioa sho@ la kichaga
 
Kutaja majina kunaharibu upelelezi, si kwa watuhumiwa wa makosa kama hayo, ama kwa majambazi, hata majambazi wakifanya tukio na kutoroka, halafu raia wakachoma majina yao, huwa hawatajwi, maana anaweza sikia ama kuona tangazo la majina, akawaambia wakapotea.

Ila siku zote, ushahidi ukikamilika na kufikishwa mahakamani, huwa wanatajwa majina yao, ila kwa kesi kama ya watoto hao (waathiriwa), majina yao huwa hayatajwi, na hata usikilizaji wa kesi zinazohusisha watoto, huwa ni siri. Ni kwa faida ya afya ya akili na mwili ya mtoto.

Ahsante!
 
Mkuu wa dunia hii, yaani Ibilisi, anazo mbinu nyingi sana za kuwahadaa wanadamu milele yote.

Sala kwake Mungu, aliye hai ndizo hutusaidia kuondokana na mitego ya ibilisi.

Tusijidanganye ya kuwa labda unaishi maisha mazuri full security, umesoma sana wewe na familia yako yote, mchambuzi na mwanasiasa mzuri, masikini unayehitaji kusaidiwa kila mara, kama hauna nafasi ya kumpa Mungu, utukufu, heshima, kumuabudu, kumshukuru, kumsifu, na zaidi kumuomba akuepushia na madhila yote mabaya ya dunia hii, bado tu utanasika kwenye mitego ya ibilisi, kama siyo wewe, kizazi chako.

Tuwe watu wa sala, kumuomba Mungu, siku zote, tuwaombee watoto wetu, vizazi vilivyopo na vijavyo, kuepukwa na mabalaa.

Ahsante!
 
Akina Mangi wameshindwa kwenda hata Malindi wakanunua makahaba wanaamua kuwafanyia ushenzi watoto wadogo wa shule ya msingi.
 
yani hawa mimi sipeleki polisi nitawapa mateso ya ajabu kwa gharama zozote zile,.......... papuchi za watu wazima zimejaa kila mahali mtu anaenda kudandia wototo.... haki ya nani ningewahasi kwa nyundo pumbavu kabisa...
 
Tulaani vitendo hivyo kwa nguvu ya sala haswa, najua ndiyo kuna kuandamana, kupiga kelele hasa mitandaoni, kuwalaani wahusika, kutishana na mijeledi na mitutu ya bunduki, n.k n.k, ila sala siku zote tukizifanya kwa pamoja, popote pale ulipo na dini yako ama dhehebu lako, ina/linalomuamini Mungu wa kweli, tutayashinda haya.

Binafsi nawapa pole watoto hao, nikiwa kama mzazi naelewa namna inavyouma (mmemsikia babu hapo, anakosa usingizi). Watuhumiwa haki yao iwapase.

Ahsante!
 
Ushahidi wa watoto huwa hautiliwi shaka na ukitambuliwa kwenye gwaridi basi kinachofuata ni hukumu.
Hukumu ni kifongo cha maisha na kazi ngumu. Wakumie haraka ili iwe fundisho kwa wengine wanaowaharibia maisha watoto wadogo ambao wanadaganywa kwa sh 500/
Huo ni unyama wa hali ya juu na adhabu iwe kali sawa na ubaya walioufanya.
 
yani hawa mimi sipeleki polisi nitawapa mateso ya ajabu kwa gharama zozote zile,.......... papuchi za watu wazima zimejaa kila mahali mtu anaenda kudandia wototo.... haki ya nani ningewahasi kwa nyundo pumbavu kabisa...

Usishangae ukisikia wazazi wanataka kuyamaliza nyumbani. Watu wengi wanayachukulia haya mambo kirahisi rahisi mno.
 
Hayo mambo hayakuwepo zamani pale Moshi..hembu watafiti wachunguze lazima kuna sababu tu..wachaga na wapare hawakuwa na hizo mambo..Nadhani viroba pia ni chanzo kikuu
 
Back
Top Bottom