Watoto wamuua baba yao kwa fimbo

Watoto wamuua baba yao kwa fimbo

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713
JESHI la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watoto watatu, kwa tuhuma za kumpiga fimbo kichwani baba yao mzazi na kumsababishia kifo. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Gilles Muroto, alisema tukio hilo ni la mwezi Septemba 15, mwaka huu katika Kijiji cha Mkunyu Kata ya Kikukuru Tarafa ya Mabira wilayani Kyerwa.

Alisema siku ya tukio, watuhumiwa hao, ambao hakuwataja majina yao kutokana na umri wao kuwa chini ya miaka 18, walimuua baba yao, Henry Siliakus (62) kwa kumchapa fimbo kichwani akiwa nyumbani kwake hadi akapoteza uhai wake.

Muroto alisema watoto hao, mmoja wao ana umri wa miaka 17, anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Mkunyu.
Mwingine ana umri wa miaka 13, anasoma darasa la nne. Mwingine ana umri wa miaka 11, anasoma darasa la tatu. Wote wawili wanasoma katika Shule ya Msingi Mkunyu.

Kamanda alisema sababu ya awali ya mtafaruku huo, uliosababisha kifo ni ugomvi wa baba na watoto wake, kwa kile kinachodaiwa baba yao kuwa na tabia ya kuuza chakula cha familia na kuwaacha wakitaabika na njaa.

Kamanda alisema jeshi hilo, bado linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na litawafikisha mahakamani watoto hao pale taratibu za kisheria zitakapokamilika.

CHANZO: Habari Leo
 
...tabiaya
kuuzachakula
chafamilia
nakuwaacha
wakitaabika
nanjaa...

Mmmmmmmh!
 
Ukute hapo watoto wanalikuwa wanalima kwa nguvu zote, wakivuna dingi anaanza kukwapua, ananywea pombe na kuja kuwafumua akiwa amelewa wakati wao wanapiga miayo kwa njaa, dunia hii kuna majaribu sana, kama mimi ni hakimu hapo nawapa adhabu ya bakora nne nne tu!
 
Njaaaa....! Ni shida! Njaa huondoa subira Na busara. Hiyo imesababishwa Na ghadhabu ya Njaa.
JESHI la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watoto watatu, kwa tuhuma za kumpiga fimbo kichwani baba yao mzazi na kumsababishia kifo. Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, Gilles Muroto, alisema tukio hilo ni la mwezi Septemba 15, mwaka huu katika Kijiji cha Mkunyu Kata ya Kikukuru Tarafa ya Mabira wilayani Kyerwa.

Alisema siku ya tukio, watuhumiwa hao, ambao hakuwataja majina yao kutokana na umri wao kuwa chini ya miaka 18, walimuua baba yao, Henry Siliakus (62) kwa kumchapa fimbo kichwani akiwa nyumbani kwake hadi akapoteza uhai wake.

Muroto alisema watoto hao, mmoja wao ana umri wa miaka 17, anasoma kidato cha pili katika Shule ya Sekondari ya Mkunyu.
Mwingine ana umri wa miaka 13, anasoma darasa la nne. Mwingine ana umri wa miaka 11, anasoma darasa la tatu. Wote wawili wanasoma katika Shule ya Msingi Mkunyu.

Kamanda alisema sababu ya awali ya mtafaruku huo, uliosababisha kifo ni ugomvi wa baba na watoto wake, kwa kile kinachodaiwa baba yao kuwa na tabia ya kuuza chakula cha familia na kuwaacha wakitaabika na njaa.

Kamanda alisema jeshi hilo, bado linaendelea na uchunguzi wa kina juu ya tukio hilo na litawafikisha mahakamani watoto hao pale taratibu za kisheria zitakapokamilika.

CHANZO: Habari Leo
 
ningekuwa hakimu hata hivyo viboko nisingewahukumu. zaidi ningewaambia adhabu yao ni kwenda kupanda miti kuzunguka shamba lao na kuimwagilia maji. basi.
maana mizazi mingine ni sheeda kwenye dunia hii.

Back
Top Bottom