Watoto wa mgombea Ubunge Eldoret-Kenya watekwa na kuuawa Kenya

Bowie

JF-Expert Member
Sep 17, 2016
4,372
6,078
Watoto 3 wa mgombea ubunge huko Eldoret Kenya ambao walikuwa wamepotea wamekutwa wameuawa na maiti zao kutupwa kwenye mto Nzoia. Watoto hao walipotea toka jumamosi iliyopita wakati wakitoka kanisani (Eldovil SDA Church).
IMG_0227.JPG

Mgombea huyo ambaye watoto wake wameuawa anaitwa jina James Ratemo wa Jubilee.
Na mgombea Udiwani huko Machakos Thomas Minito amekutwa ameuawa na maiti take kutupwa Athi River huko machakos.
 
Mi nalijua Kenya mme-grow up na mko na akili mingi plus true democracy kupita manji mengine Africa Mashariki na Kati kumbe bado iko na mambo ya kutekana na kuua kama alshabab
 
Kweli Inasikitisha sana
lakini kwa kipindi jama hiki
kenya haya mambo niyakawaida kutokea
Hili si Geni
japo huu ni unyama ulio pitiliza
watoto wadogo sana hao!!
 
ndugu zetu WAKENYA acheni siasa za chuki!!! mtakwisha wote!!! hebu kuweni na ubinaadamu angalau kidogo!!!
fanyeni siasa za kistaarabu kwa masĺahi ya nchi yenyu.
 
Na hii ndiyo watu hapa jukwaani wanaisifia kuwa, Kenya wana demokrasia nzuri kuliko ya Tanzania!
================
R.I.P watoto wa James Ratemo wa Jubilee. Pia R.I.P mgombea Udiwani huko Machakos Thomas Minito. Poleni sana wafiwa.
Hilo la demokrasia nzuri wala halina mjadala na usiliwe hapa. Watu kupanga njama za kuuana au kuteka watu mbona Tanzania ni kinara? Mmesahau, Igunga, Arumeru?
 
Back
Top Bottom