Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,618
- 9,607
Watoto 3 kati ya 4 wanaishi katika nchi ambako upatikanaji wa chanjo ni mdogo na kusababisha milipuko ya magonjwa: WHO/UNICEF
Viwango vya chanjo za utotoni ulimwenguni vilikwama mwaka 2023 na na kuacha watoto milioni 2.7 zaidi bila chanjo au kiwango kisichotosheleza cha chanjo ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizochapishwa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF.
Makadirio ya hivi karibuni ya WHO na UNICEF ya utoaji wa chanjo kitaifa (WUENIC) ambayo hutoa kiwango kikubwa zaidi cha takwimu duniani kuhusu mwelekeo wa chanjo dhidi ya magonjwa 14 yanasisitiza haja ya jitihada zinazoendelea za kujikwamua, kurejesha na kuimarisha mifumo ya chanjo.
"Mienendo ya hivi karibuni inaonyesha kwamba nchi nyingi zinaendelea kukosa chanjo kwa watoto wengi," amesema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell na kuongeza kuwa "Kuziba pengo la chanjo kunahitaji juhudi za kimataifa, serikali, washirika, na viongozi wa eneo hilo kuwekeza katika huduma za afya ya msingi na wwahudumu wa jamii ili kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo, na kwamba huduma ya afya kwa ujumla inaimarishwa."
Hata hivyo, idadi ya watoto ambao hawakupokea hata dozi moja ya chanjo hiyo iliongezeka kutoka watoto milioni 13.9 mwaka 2022 hadi milioni 14.5 mwaka 2023.
WHO na UNICEF wanasema “Zaidi ya nusu ya watoto ambao hawajachanjwa wanaishi katika nchi 31 zenye mazingira magumu, zilizoathiriwa na migogoro na mazingira hatarishi, ambapo watoto wako katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa sababu ya changamoto na ukosefu wa usalama, lishe na huduma za afya.”
Zaidi ya hayo, watoto wengine milioni 6.5 hawakukamilisha dozi yao ya tatu ya chanjo ya DTP, ambayo ni muhimu kufikia ulinzi wa magonjwa kwa watoto wachana na umri wa utotoni.
Kwa mujibu wa takwimu hizo mienendo hii ambayo inaonyesha kuwa utoaji wa chanjo kimataifa haujakuwa na mabadiliko tangu mwaka 2022 na cha kushangaza zaidi bado haujarejea katika viwango vya 2019, inaonyesha changamoto zinazoendelea na usumbufu wa huduma za afya, changamoto za vifaa, kusita kwa watu kupokea chanjo na ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma.
Takwimu zinaonyesha zaidi kwamba viwango vya chanjo dhidi ya ugonjwa hatari wa surua vilikwama, na kuwaacha karibu watoto milioni 35 bila ulinzi wowote au sehemu tu.
Mwaka wa 2023, ni asilimia 83 tu ya watoto duniani kote ndio walipata dozi yao ya kwanza ya chanjo ya surua kupitia huduma za kawaida za afya, wakati idadi ya watoto wanaopokea dozi yao ya pili iliongezeka kwa kiasi kutoka mwaka uliopita, na kufikia asilimia 74 ya watoto.
Takwimu hizi hazifikii kiwango cha asilimia 95 kinachohitajika kuzuia milipuko, kuzuia magonjwa na vifo visivyo vya lazima, na kufikia malengo ya kutokomeza surau yamesema mashirika ya WHO na UNICEF
Katika kipindi cha miaka mitano iliyopita, milipuko ya surua ilikumba nchi 103 ambazo ni nyumbani kwa takriban robo tatu ya watoto wachanga duniani.
UN News
Viwango vya chanjo za utotoni ulimwenguni vilikwama mwaka 2023 na na kuacha watoto milioni 2.7 zaidi bila chanjo au kiwango kisichotosheleza cha chanjo ikilinganishwa na viwango vya kabla ya janga la COVID-19 mwaka 2019, kwa mujibu wa takwimu mpya zilizochapishwa leo na Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto duniani UNICEF.
Makadirio ya hivi karibuni ya WHO na UNICEF ya utoaji wa chanjo kitaifa (WUENIC) ambayo hutoa kiwango kikubwa zaidi cha takwimu duniani kuhusu mwelekeo wa chanjo dhidi ya magonjwa 14 yanasisitiza haja ya jitihada zinazoendelea za kujikwamua, kurejesha na kuimarisha mifumo ya chanjo.
"Mienendo ya hivi karibuni inaonyesha kwamba nchi nyingi zinaendelea kukosa chanjo kwa watoto wengi," amesema Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF Catherine Russell na kuongeza kuwa "Kuziba pengo la chanjo kunahitaji juhudi za kimataifa, serikali, washirika, na viongozi wa eneo hilo kuwekeza katika huduma za afya ya msingi na wwahudumu wa jamii ili kuhakikisha kila mtoto anapata chanjo, na kwamba huduma ya afya kwa ujumla inaimarishwa."
Watoto milioni 14.5 walikosa chanjo 2023
Kulingana na matokeoya utafiti wa takwimu hizo , idadi ya watoto waliopokea dozi tatu za chanjo dhidi ya diphtheria, pepopunda na pertussis (DTP) mwaka 2023 ambayo ni ishara muhimu ya chanjo ya kimataifa ilikwamia kwenye asilimia 84 sawa na watoto milioni 108.Hata hivyo, idadi ya watoto ambao hawakupokea hata dozi moja ya chanjo hiyo iliongezeka kutoka watoto milioni 13.9 mwaka 2022 hadi milioni 14.5 mwaka 2023.
WHO na UNICEF wanasema “Zaidi ya nusu ya watoto ambao hawajachanjwa wanaishi katika nchi 31 zenye mazingira magumu, zilizoathiriwa na migogoro na mazingira hatarishi, ambapo watoto wako katika hatari ya kupata magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa sababu ya changamoto na ukosefu wa usalama, lishe na huduma za afya.”
Zaidi ya hayo, watoto wengine milioni 6.5 hawakukamilisha dozi yao ya tatu ya chanjo ya DTP, ambayo ni muhimu kufikia ulinzi wa magonjwa kwa watoto wachana na umri wa utotoni.
Kwa mujibu wa takwimu hizo mienendo hii ambayo inaonyesha kuwa utoaji wa chanjo kimataifa haujakuwa na mabadiliko tangu mwaka 2022 na cha kushangaza zaidi bado haujarejea katika viwango vya 2019, inaonyesha changamoto zinazoendelea na usumbufu wa huduma za afya, changamoto za vifaa, kusita kwa watu kupokea chanjo na ukosefu wa usawa katika upatikanaji wa huduma.
Ufikiaji mdogo wa chanjo tayari unachochea milipuko ya surua