RUCCI
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 1,701
- 1,714
Watoto wawili wa familia moja wamekufa na wengine watano akiwemo mama yao wamenusurika, baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuangukiwa na kuta, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa zaidi ya saa moja wilayani Manyoni.
Akithibitisha kutokea kwa vifoo hivyo mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Manyoni Daktali Kitundu Jackson amekiri kupokea maiti hizo ambazo zimeangukiwa na nyumba eneo la kitongoji cha kipondoda na kuwataja walio kufa ni Amina Ashery miaka saba na Emily Ashery miaka minne.
Akieleza huku akiwa na majonzi mama watoto hao wawili walio kufa akiwa pamoja na watoto wengine watano walionusurika, amesema alikuwa amelala yeye na familia yake na gafla alisikia kishindo na akafunikwa na kifusi cha udongo ndipo alipoanza kuomba msaada, baada ya kutolewa watoto wawili wakiwa katika hali mbaya na walipofika hospitali walikuwa tayari wamesha fariki.
Kwa upande wake mkurugenzi wa mamlaka ya mji mdogo wilayani Manyoni Bwana Yona Chalinze, amesema wao kama mamlaka walisha toa taarifa kwa wenye viti wa mitaa kuwa watu wanao ishi mabondeni kuchuwa taadhari kutokana na mvua kubwa zitakazo nyesha ,huku naye pia bi. Eliza mjengi ambaye yeye alishuhudia alikuwa na haya yakusema.
Chanzo: ITV