Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Moshi Vijijini mkoani Kilimanjaro, Ramadhan Mahanyu amepiga marufuku matumizi ya mabango na vipeperushi vya watiania ubunge katika majimbo ya Moshi Vijijini na Vunjo.
Mahanyu ametoa agizo hilo leo Jumatano, Julai 30, 2025, wakati wa mikutano ya kuwatambulisha wagombea saba wa Moshi Vijijini katika kata za Kibosho Mashariki, Uru Kusini na Uru Kaskazini. Wagombea hao ni Profesa Patrick Ndakidemi, Moris Makoi, Victor Tesha, Deogratius Mushi, Felister Njau, Salim Kikeke na Wilhad Kitaly.
Mahanyu amesema marufuku hiyo inahusu pia wapambe wa wagombea kubeba mabango au vipeperushi vyenye picha au majina ya watia nia, akibainisha kuwa hatua hiyo inalenga kuzuia viashiria vya rushwa kabla ya kura za maoni za CCM Agosti 4, 2025.
Amesema wagombea wataruhusiwa kutumia mabango baada ya chama kuwapitisha rasmi kupeperusha bendera. Wagombea hao walipewa nafasi ya kujitambulisha, kueleza sera na kujibu maswali ya wajumbe, huku wakiahidi kuboresha barabara, maji, shule, mikopo nafuu na huduma za afya.