GE2025 Watia Nia Wawili wa ubunge matatani Kwa kutoa Rushwa Kwa wajumbe

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke, Holle Makungu, amesema kuwa katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu, taasisi hiyo imewahoji na kuwaachia kwa dhamana watia nia wawili wa nafasi ya Ubunge katika Majimbo mawili tofauti kwa tuhuma za kushawishi na kutoa rushwa kwa Wajumbe wa Chama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makungu amesema kuwa watia nia hao ambao majina yao yanaifadhiwa wametuhumiwa kujaribu kushawishi wajumbe kwa kutoa fedha kwa lengo la kuhakikisha majina yao yanapendekezwa na vikao vya maamuzi vya Chama tawala ili kushiriki katika kura za maoni.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na TAKUKURU ulibaini dalili za vitendo vya rushwa, na kwa mujibu wa taratibu, taarifa hizo ziliwasilishwa kwa chama husika ambacho tayari kimechukua hatua kwa kutorejesha majina yao katika orodha ya watakaoshiriki kura za maoni,” amesema Makungu.

Aidha, ameongeza kuwa uchunguzi wa kina bado unaendelea na hatua zaidi za kisheria zinaweza kuchukuliwa iwapo ushahidi zaidi utapatikana. “Tunawakumbusha Wagombea wote kuwa vitendo vya rushwa vinaweza kusababisha si tu kufutiwa nafasi ndani ya chama, bali pia kuchukuliwa hatua kali za kisheria hata kama mtu ataongoza katika kura za maoni,” amesisitiza.

Katika kuelimisha umma, Makungu amekumbusha kuwa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, sambamba na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010, pamoja na marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2024, zinapiga marufuku vikali vitendo vya rushwa katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.
 
View attachment 3427251
Hao wanawaonea tu,Rushea ipo hadi juu na imeshuka hadi kwa watia nia wa kata.
 
Kazi iendelee kuanzia ngazi ya kata hadi juu..muwe mnatupatia taarifa kama hzi sisi wananchi ili tuanze kurudisha imani kwa chombo hiki cha TAKUKURU.
 
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke, Holle Makungu, amesema kuwa katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu, taasisi hiyo imewahoji na kuwaachia kwa dhamana watia nia wawili wa nafasi ya Ubunge katika Majimbo mawili tofauti kwa tuhuma za kushawishi na kutoa rushwa kwa Wajumbe wa Chama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 1,2025 jijini Dar es Salaam, Makungu amesema kuwa watia nia hao ambao majina yao yanaifadhiwa wametuhumiwa kujaribu kushawishi wajumbe kwa kutoa fedha kwa lengo la kuhakikisha majina yao yanapendekezwa na vikao vya maamuzi vya Chama tawala ili kushiriki katika kura za maoni.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na TAKUKURU ulibaini dalili za vitendo vya rushwa, na kwa mujibu wa taratibu, taarifa hizo ziliwasilishwa kwa chama husika ambacho tayari kimechukua hatua kwa kutorejesha majina yao katika orodha ya watakaoshiriki kura za maoni,” amesema Makungu.

Aidha, ameongeza kuwa uchunguzi wa kina bado unaendelea na hatua zaidi za kisheria zinaweza kuchukuliwa iwapo ushahidi zaidi utapatikana.

“Tunawakumbusha Wagombea wote kuwa vitendo vya rushwa vinaweza kusababisha si tu kufutiwa nafasi ndani ya chama, bali pia kuchukuliwa hatua kali za kisheria hata kama mtu ataongoza katika kura za maoni,” amesisitiza.

Katika kuelimisha umma, Makungu amekumbusha kuwa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, sambamba na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010, pamoja na marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2024, zinapiga marufuku vikali vitendo vya rushwa katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.
 
Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke, Holle Makungu, amesema kuwa katika kipindi cha Aprili hadi Juni mwaka huu, taasisi hiyo imewahoji na kuwaachia kwa dhamana watia nia wawili wa nafasi ya Ubunge katika Majimbo mawili tofauti kwa tuhuma za kushawishi na kutoa rushwa kwa Wajumbe wa Chama.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Makungu amesema kuwa watia nia hao ambao majina yao yanaifadhiwa wametuhumiwa kujaribu kushawishi wajumbe kwa kutoa fedha kwa lengo la kuhakikisha majina yao yanapendekezwa na vikao vya maamuzi vya Chama tawala ili kushiriki katika kura za maoni.

“Uchunguzi wa awali uliofanywa na TAKUKURU ulibaini dalili za vitendo vya rushwa, na kwa mujibu wa taratibu, taarifa hizo ziliwasilishwa kwa chama husika ambacho tayari kimechukua hatua kwa kutorejesha majina yao katika orodha ya watakaoshiriki kura za maoni,” amesema Makungu.

Aidha, ameongeza kuwa uchunguzi wa kina bado unaendelea na hatua zaidi za kisheria zinaweza kuchukuliwa iwapo ushahidi zaidi utapatikana. “Tunawakumbusha Wagombea wote kuwa vitendo vya rushwa vinaweza kusababisha si tu kufutiwa nafasi ndani ya chama, bali pia kuchukuliwa hatua kali za kisheria hata kama mtu ataongoza katika kura za maoni,” amesisitiza.

Katika kuelimisha umma, Makungu amekumbusha kuwa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2024, sambamba na Sheria ya Gharama za Uchaguzi ya mwaka 2010, pamoja na marekebisho ya Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ya mwaka 2024, zinapiga marufuku vikali vitendo vya rushwa katika hatua zote za mchakato wa uchaguzi kabla, wakati na hata baada ya uchaguzi.

View attachment 3427251
Wasiwaonee hiyo ni jadi juu mpaka chini!! Tuishi nalo tu.
 
Back
Top Bottom