watawala na polisi someni alama za nyakati | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

watawala na polisi someni alama za nyakati

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nkisumuno, Sep 8, 2012.

 1. n

  nkisumuno JF-Expert Member

  #1
  Sep 8, 2012
  Joined: May 22, 2012
  Messages: 209
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Natoa wito kwa watawala na polisi wa Tanzania kusoma alama za nyakati kuhusiana na mabadiliko yanayopamba moto.
  kama ilivyo kawaida watu kubisha na kutokubali ukweli japo unajulikana wapo watakaobisha.

  Hakuna wakati ambao kumetokea vuguvugu la mabadiliko kama ilivyo kwa Tanzania leo. Watawala wanalijua, CCM inajua na hata polisi wanalijua hilo kuthibitisha hilo ni pamoja na nguvu zinazotumika kudhibiti mabadiliko hayo, Msajili na kada wa CCM Tendwa naye analijua hilo na ndiyo maana anakimbilia kuitisha CHADEMA kuwa atakifuta.

  Wito wangu naomba watawala wakubaliane na wakati vinginevyo Taifa litapelekwa pabaya kuliko kawida. Tangu polisi walipoamua kuua na ndivyo watanzania wanavyozidi kuongezeka kwenye mikutano na maandamano. Naomba watawala waache mara moja vitisho kama wanaweza wajibu hoja, watanzania wa leo sio wale wa jana.Mbinu zozote zinazopangwa na watawala Chadema wanazipata. Kabla ya tamko la tendwa kuliwekwa uzi hapa kuhusu sababu za polisi kuua katika mikutano ya chadema sababu mojawapo ni kutaka kupata sababu za kukifuta Chadema siku chache baadaye Tendwa akatoa tamko kama kupima upepo

  Ushauri wangu kwa Tendwa asijaribu kufanya hivyo maana akifanya hivyo ajue kutatokea machafuko ya ajabu kwani kwa sasa Chadema ni zaidi ya CCM. CCM wanatumia mbinu zile za zamani wakati watanzania wamebadilika, Hivyo nawaomba watawala waache mbinu chafu vinginevyo haya yatakuja wahukumu. Polisi acheni kusikiliza amri haramu za CCM kwa kuua watanzania wasio na hatia damu zao zitawalilia. Kwa damu iliyomwagika ya raia haiwezi kwenda bure hivyo CCM jiandaeni kukabidhi madaraka muda ukifika.

  Polisi mkiendelea kuua ni ole wenu maana mnaua na jioni mnakuwa na watanzania haohao mnawaua, watoto wenu wanasoma na watoto wa wale wale mnaowaua sasa sijui pale watanzania watakapoamua kujibu mapigo, hatupendi tufike huko. Kumbukeni madikiteta waliotangulia leo hii wako wapi, Kikwete naomba muogope Mungu na ili ujisafishe wawajibishe waliomuua mwangosi hata kama walipokea amri toka chama chako. Watanzania hatuna imani na IGP MWEMA, Waziri Nchimbi na jeshi lote la polisi. Tume ya Nchimbi inachunguza nini wakati kila kitu kipo wazi.

  Wako wapi magangwe kama Id Amin, Mabutu, Ghadafi na wengine wengi tujifunze kwa hao kuwa ubabe na fahari ya dunia ni ya kitambo tu, kuua kwa makusudi inauma, Watanzania tuombee Taifa hili ili Mungu alinusuru.
   
 2. a

  adolay JF-Expert Member

  #2
  Sep 8, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,567
  Likes Received: 3,026
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nkisumuno umewapa tahadhali mahsusi, bahati mbaya wamesahau kauli ya Hayati mwl Nyerere 'kula nyama ya mtu ni laana, ukishakuila hutaacha bali utafanya mazoea' sasa imewarudi kuua raia kwao sio tatizo tena kwa sababu shetan amewabeba.

  Badala ya kumtafuta mchawi kwa cdm serikali itambue mchawi ni sekali na ccm yake

  -kushindwa kwa sera za ccm, (hazitekelezeki - Mkapa)

  -Ahadi nyingi za uwongo na utapeli. (Kama watazitekeleza watanzania watawamin)

  -mbinu chafu za kutugawa watanzania (udin, ukabila na ukanda - hakuna ukweli ni propaganda chafu)

  -kukumbatia mafisadi na ufisadi (raia wanasikia na wanaona lazima wachukie)

  -Huduma mbovu kwa jamii (Afya, Elimu na miundombinu vyote ovyo kabisa.

  Nk, nk.

  Kibaya ccm na serikali yake wamelala fofo, kizazi hiki sio kile cha kukubali kila kitu. Tunahoji, tunadadis na kutafakali kabla ya kusema zidumuuu! Matokeo yake inakuwa hapana mnatuibia na kutudanganya hatutaki.

  Ni jukum la ccm na sekali yake kujichunguza na kurekebesha makosa.
   
 3. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #3
  Sep 8, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Kikwete na mbwembwe zake za 2005 za maisha bora na usalama wa nchi.....kila kitu kimemshinda amebaki anambwelanbwela tu mambo hayaendi......kudadeki kabaki kuwa promota
   
 4. B

  Bahati Risiki JF-Expert Member

  #4
  Sep 8, 2012
  Joined: Jun 20, 2012
  Messages: 531
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wazee wa makengeza, vicheko, ushemeji wana habari na alama za nyakati? Kwao cha maana ni udoctor feck. Yale walioyaahidi yamewashinda sasa wanaishia kutishia, kutesa, na kuuwa. Kuna mtu amesema huwezi kuwapiga risasi nyuki wote kwenye mzinga. Ni lazima wachache watakukimbia tu. Kwa sasa wale walioukimbia mzinga ndiyo wanamshambulia daktar feck.
  Huyu hajakaa darasani kapambana na zile statistics za udokta. Hajawahi kuianalize hata case study yenyewe sasa ataongozaje nchi? Hizi alama za nyakati ni kubwa kuliko yeye. Mtoto mdogo hawezi kuelewa ukubwa wa mlima Kilimanjaro. Either atauona mkubwa kuliko yeye au mdogo sana kiasi ashindwe hata kuuogopa. Huyu JK ni mtoto anayechekea watanzania wakati wanadai haki zao kwa nguvu zao zote. Kicheko chake kitageuka kilio very soon!
   
Loading...