Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
Nafikiria hii kauli kutaka kujua Mheshimiwa alikuwa anamaanisha nini. bado sijafahamu sawa sawa.
Kwahiyo tunatawaliwa hatuongozwi? Kuna tofauti kubwa kati ya kutawaliwa na kuongozwa.
Watu wanaoongozwa wana kauli dhidi ya serikali yao. Watu wanaotawaliwa hawana.
Kwa kauli kama hii inaonyesha kuna tatizo katika demokrasia yetu kama viongozi na CCM wana fikra kama hizi. Inaonyesha pia uhuru wa watu wetu bado uko mashakani.
Watu huru hawatawaliwi wanaongozwa. Fikra hizi sio nzuri sana kama tunataka kujenga demokrasia ya kweli na yenye misingi iliyobora. Nchi hii haiko kwaajili ya kundi fulani la watu. Nchi hii ni ya wote na raia wa nchi hii wana haki ya kuchagua watu gani wawaongoze.
Kuwepo madarakani kusiwasahaulishe na kudhani wanawamiliki watanzania kama ng'ombe. Watanzania ni binadamu wana uhuru na maamuzi ya kuchagua ni watu gani wawaongoze.
Nadhani hii habari ya kujiita watawala sio nzuri. Kwasababu katika nchi hii hakuna watu waliozaliwa kusudi wawatawale wengine. Kila mtu ana haki ya kuwa kiongozi wa nchi hii ikiwa ni raia wa taifa hili mwenye akili timamu na uwezo wa kuongoza.
Na wananchi wa Tanzania ndio wenye kauli ya mwisho ya nani awaongoze. Kwahiyo kama ni vyama vya ovyo ovyo wananchi ndio wanaojua sio wewe Magufuli. Wananchi wakisema wamesema hata kama wewe ni mzuri kiasi gani kama wamekukataa wamekukataa . Ni muhimu kama tumeamua kuwa nchi ya kidemokrasia tukaheshimu demokrasia. Wananchi wamekuchagua wewe sio uwe mtawala bali kiongozi wao.
Ni muhimu uhuru wa watu ukalindwa. Uhuru wa kuongea, wa kuandika machapisho na vitabu, uhuru wa kukutana na watu na kutoa mawazo kwa uhuru, uhuru wa kufanya mikutano ya hadhara. Nahofu sana na uhuru huu kutoweka kama viongozi bado wana dhana ya wao ni watawala dhidi ya wananchi. Nisingependa hali hii iwepo katika nchi hii. Uhuru wa watu ni muhimu sana ndio unaofanya taifa liendelee. Taifa lolote linalokandamiza mawazo ya watu haliwezi endelea.
Sitaki kumkatisha tamaa na wala sipingi hatua anazochukua dhidi ya ufisadi , kubana matumizi ya serikali na ukusanyaji wa kodi , nampongeza kwa hilo. Lakini tunapaswa kusema pale kunapokuwepo na kasoro. Ili kumsaidia yeye pamoja na nchi yetu. Kila mtu anapenda nchi hii iendelee. Lakini demokrasia ya nchi hii ni muhimu pia. Inapaswa kulindwa ili ikue bado changa mno na watu wetu bado wachanga katika mfumo huu wa demokrasia.
Ningependa hii kauli ibadilishwe kwasababu hakuna mtu wala chama chenye haki miliki ya hii nchi. Hii nchi ni ya watanzania wote. Sio ya CCM wala CHADEMA au vyama vingine. Vyama hivi vinapata haki ya kuongoza nchi kutoka kwa watu na sio haki ya kuwatawala. Kusimamia haki kwa watu wote na misingi ya sheria na katiba. Lengo letu ni kujenga Tanzania moja isiyogawanyika kimatabaka ya watawala na watawaliwa.
Kama wana mawazo kama haya wakishindwa uchaguzi sidhani kama wanaweza kuachia dola. Na kama wasipoachia dola hali ya amani ya nchi yetu itakuwaje? Wapinzani wa nchi hii wana haki sawa na chama kilichopo madarakani . Misingi hii ya demokrasia inapaswa kulindwa kwaajili ya amani ya nchi yetu.
Natambua siasa zetu zina matatizo zinahitajika kuwa reformed. Kwasababu ni muhimu kujenga siasa zenye misingi ya kuheshimiana. Zinazojadilia issues na zenye mantiki zaidi. Kwasababu taifa hili litaboreka pale tu siasa zetu zitakapokuwa bora.
Hongera sana kwa hatua unazochukua katika kukusanya kodi. Kudhibiti rushwa na ufisadi. kubama matumizi katika serikali. Ni kazi ngumu inayohitaji busara na hekima pamoja na ushawishi na sio nbguvu peke yake. Mimi ni miongoni mwa watu wanaoamini kwamba watu wanaweza kubadilika na nguvu pekee haiwezi kusaidia pasipo kuangalia mambo mengine. Na kushawishi watu kwamba tunahitaji kubadilika kwa faida ya taifa letu.
Mabadiliko ya tabia za watu wetu yanahitaji nguvu za pamoja. Serikali pekee kwa kutumia nguvu haiwezi kubadilisha watu. Familia zizingatie maadili, watoto wetu wapewe elimu bora na kufunzwa nidhamu na adabu. Watu wa dini wafanye kazi yao vizuri kuhubiria watu waache uovu na mwisho kabisa serikali isimamie sheria. Ni muunganiko wa vitu vitatu.
Wazazi katika familia lazima wazingatie misingi ya maadili na kwa pamoja kujenga jamii zilizobora na zenye adabu na nidhamu. Watoto wetu wapewe elimu bora na yenye maadili. Watu wa dini wahubirie watu kikamilifu waache uovu na serikali isimamie sheria kikamilifu. Serikali haiwezi kufanya kazi peke yake pasipo mihimili hii mingine. Ufisadi utaondoka kama jamii nzima itashiriki kikamilifu kwa kuuchukia na kutaka kuuondoa ufisadi nafsini mwao.
Ni muhimu hoja zikashinda na kutawala wakati wowote taifa litakapokuwa na sintofahamu. Kwasababu kama taifa tunatafuta ukweli ambao utalipeleka taifa hili mbele. Hatuwezi kuishi katika uongo alafu tuakadhani tutaendelea kama taifa. Ukweli haupaswi kukandamizwa. Ni kama kufukia kuni za moto kwenye ardhi moshi utatoka tu. Tushindanishe hoja na ukweli utakapopatikana ukweli huo ndio utumike kulipeleka taifa mbele. Na ukweli ni kwamba kama taifa tunapaswa kubadilika na kufanya yaliyosahihi kwa taifa letu bila kuangalia ubinafsi. Bila kuangalia familia yako au kundi unalotoka katika jamii.
Mwisho pamoja na wananchi ni Mungu ambaye humweka yeyote atakaye madarakani kwahiyo sio vyema kujinyanyua hivyo. Katika biblia kuna hadithi ambazo zinaonyesha watu walioinuliwa kutoka katika mavumbi na kutwaa ufalme. Kina Mfalme daudi na wengineo. Kujishusha ni bora zaidi.
PSALM 113 : 7- 9
He lifts the poor from the dust
and the needy from the garbage dump.
He sets them among princes,
even the princes of his own people!
He gives the childless woman a family,
making her a happy mother.
Tunapofanikiwa tukumbuke tulikotoka. Tujinyenyekeshe kwasababu kuna Mungu aliyejuu yetu wote. Historia yote ya binadamu imejawa na maajabu ya Mungu. Nenda kasome historia za wakuu wa nchi. Walikuwa hawana kitu maskini, wajinga. Kitu kimoja tunachopaswa kujifunza hatupaswi kumsahau Mungu na kujinyayua tunapofanikiwa.