Watatu wauawa daraja la Mkapa, walikataa amri ya polisi iliyowataka wasimame

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Watu watatu wameuwa katika Daraja la Mkapa inadaiwa watu hao waliokuwa kwenye pikipiki huku wamefunika nyuso zao kisha walikataa amri ya Jeshi la Polisi iliyowataka wasimame.

====================================================

Majambazi Yakiume Yaliyokuwa Yamevaa Hijabu yauawa na Polisi

MUUNGWANA BLOG / 1 hour ago

[https://2]

Watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wameuwa kwa kupigwa risasi na polisi baada ya kukaidi amri ya kutakiwa kusimama eneo la kizuizi cha Mwembe Muhoro wilayani Rufiji, mkoani Pwani.

Watu hao walikuwa wamepakiana kwenye pikipiki moja huku wakiwa wamevaa hijabu.

Akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na tukio hilo, kamanda wa Polisi mkoani Pwani ,Onesmo Lyanga alisema pikipiki nyingine mbili zilifanikiwa kukimbia.

Akielezea juu ya tukio hilo alifafanua,lilitokea Aprili 2 mwaka huu majira ya mchana ,Muhoro ,Rufiji barabara kuu ya Dar es Salaam Lindi.

“Siku ya tukio askari walipata taarifa kuwa kulikuwa na pikipiki tatu zikitokea Kibiti kwenda mikoa ya Kusini zikiwa zimebeba watu watatu kila moja “

“Miongoni mwa pikipiki hizo kati yake mbili wamebebwa watu waliovaa hijabu,” alisema Lyanga.

Alisema askari wa barabarani walipewa taarifa katika kizuizi cha Mparange na kuwasimamisha ili wawahoji lakini walikataa na kupita ambapo waliwajulisha wenzao kwenye kizuizi cha Ikwiriri lakini walikaidi kusimama.

“Baada ya hapo walifika kizuizi cha Ikwiriri lakini bado walikaidi kusimama na kuendelea kukimbia ndipo walipofika kituo cha Muhoro “

“Hata hivyo hawakusimama na askari waliokuwa doria wakiwa kwenye gari waliwafuatilia na wakavuka daraja la Mkapa na waliwapa onyo kwa kupiga risasi hewani,” alisema Lyanga.

Aidha alibainisha baada ya hapo watu hao waliruka kwenye pikipiki na kuanza kukimbilia msituni na ndipo askari walipowapiga risasi za miguu na kiunoni na kufanikiwa kuwakamata.

“Majeruhi hao walijulikana ni wanaume hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika na walikuwa kwenye pikipiki yenye namba za usajili MC 272 BLW aina ya Boxer yenye rangi nyeusi”

“Watu hao wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kwa mwonekano wao walijaribu kuwawahisha hospitali ya Misheni ya Mchukwi,” alisema Lyanga.

Lyanga alisema walipofikishwa hospitali daktari alithibitisha kuwa watu hao wamefariki dunia .

Hata hivyo majina yao hayakuweza kufahamika huku pikipiki nyingine mbili zilitoroka na kuelekea mkoa wa Lindi na taarifa zimetolewa polisi ili wawakamate.

Aliwataka wananchi kuwa watulivu pale wanaposimamishwa na askari polisi badala ya kujaribu kutoroka na kwa sasa jeshi hilo limeimarisha doria katika kukabiliana na uhalifu.

C & P
 
Ukiwa kwenye pikipiki si ajabu kujifunika uso kutokana na Upepo mkali! Kutokusimama darajani ni utiifu wa sheria!! Kama walisimamishwa darajani na wakakaidi agizo hilo walikuwa sahihi! Kuna sababu nyingine yoyote? Kama hakuna sababu nyingine basi huu ni wakati kwetu sote kupambana na hizi amri za hovyo za watu waliobeba bunduki!! Kwa tunacholazimishwa kuamini eti ni amri halali za polisi!! Je wakiwa si polisi? Polisi anasimamisha gari/pikipiki darajani? Polisi wasio na sare za kipolisi wanamkamata makamu wa rais wa TLS! Wanaombwa wajitambulishe badala yake wanamweka sero!!
 
Ukiwa kwenye pikipiki si ajabu kujifunika uso kutokana na Upepo mkali! Kutokusimama darajani ni utiifu wa sheria!! Kama walisimamishwa darajani na wakakaidi agizo hilo walikuwa sahihi! Kuna sababu nyingine yoyote? Kama hakuna sababu nyingine basi huu ni wakati kwetu sote kupambana na hizi amri za hovyo za watu waliobeba bunduki!! Kwa tunacholazimishwa kuamini eti ni amri halali za polisi!! Je wakiwa si polisi? Polisi anasimamisha gari/pikipiki darajani? Polisi wasio na sare za kipolisi wanamkamata makamu wa rais wa TLS! Wanaombwa wajitambulishe badala yake wanamweka sero!!
Wabongo tupo nyuma sana kwenye masuala ya sheria na haki za raia, pia uwajibikaji wa askari hakuna..

Hivi kweli unasimamisha pikipiki darajani mwendeshaji hasimamishi basi unamdungua kwa risasi?

Hata kama walikua na intelijensia kwa ni majambazi basi kuwe na ushahidi wa fire exchange kati yao hao waliowaua kidogo kutakuwa na mantiki..

Otherwishe kamata mabashite yote yaliyohusika peleka mahakamani piga life sentence. Hawastahili kuendelea kuenjoy uraiani maana ni hatari kwa usalama wetu.
 
Back
Top Bottom