Watatu Wapandikizwa Figo Benjamin Mkapa

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2017
Posts
1,605
Reaction score
1,958


KWA mara ya pili, Hospitali ya Benjamin Mkapa ( BMH) kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) na washirika kutoka Japan wiki hii wamewafanyia upasuaji wa kupandikiza figo wagonjwa watatu.
Madaktari wawili wa kitanzania kutoka hospitali hiyo wanatarajiwa kupata mafunzo ya miezi sita kuhusiana na upasuaji wa kupandikiza figo nchini Japan. Mkurugenzi Mtendaji wa BMH, Dk Alphonse Chandika amebainisha hayo mjini hapa ambapo wagonjwa wawili wamepandikizwa figo siku ya Jumatatu na mmoja juzi.
"Upasuaji uliofanywa kwa wagonjwa hao watatu umekwenda vizuri na lengo letu ni kuhakikisha tunafanya operesheni za aina hii kila mwezi.
"Tunajua tukiongeza muda wa kufanya upasuaji wa kupandikiza figo kila mwezi itasaidia serikali kuokoa fedha nyingi ambazo wangezitumia kuwapeleka wagonjwa kupata tiba hii nje ya nchi,"amesema.
Machi mwaka huu, kwa mara ya kwanza Hospitali ya Benjamin Mkapa ilifanya upasuaji wa kupandikiza figo kwa mgonjwa mmoja, hivyo kuifanya kuwa hospitali ya pili kwa kutoa huduma hiyo baada ya ile ya Taifa ya Muhimbili(MNH).
Dk Chandika amesema madaktari kutoka Japan ambao wameungana na madaktari wa BMH kufanya upasuaji huo ni kutoka taasisi ya Tokushukai Medical Group, ambao wameingia mkataba wa makubaliano na UDOM.
Amesema kwa sasa kumekuwapo ongezeko la magonjwa yasiyoambukiza hapa nchini ambalo linachangiwa na aina ya maisha kwa wananchi.
Dk Chandika alibainisha kuwa miongoni mwa magonjwa yasiyoakuambuzika ambayo yamekuwa ni tishio ni kiharusi, saratani na figo.
TSN
 
Hizi ndio habari za kutupasha lkn za kumpigia mapambio jiwe hazina dili.
Hongereni nyote mliofanikisha maana kwasasa figo ni ugonjwa mkubwa kwa watu wengi especially walevi wa pombe Kali .
Wanakunywa pombe nyingi feki zikiwa na stika za Tra km ni halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kweli, mmoja wa waliofanyiwa namfahamu na ni Ndugu, hajawai kunywa hata pombe ya aina yeyote. Ni maradhi tu Ndugu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…