Watatu wahukumiwa kunyonga........

Mbonea

JF-Expert Member
Jul 14, 2009
640
20




Thursday, September 24, 2009 10:31 AM
MAHAKAMA KUU maalum ya Kahama Shinyanga jana iliwahukumu adhabu ya kunyongwa hadi kufa washitakiwa watatu waliopatikana na kosa la kuua motto aliyekuwa na ulemavu wea ngozi aliyekuwa akiitwa Matatizo Dunia [13].


Waliohukumiwa adhabu hiyo wakiwemo ndugu wawili wa familia moja ambao ni Emmanuel Masangwa [28] mkazi wa Hunyihuna, Chales Masangwa [42 na mwenzao Masumbuko Madata [32] mkazi wa Kitunga wilayani Bukombw mkani Shinyanga.

Adhabu hiyo ilitolewa jana na Jaji Mkuu Kiongozi wa Mahakama hiyo Gabriel Wakibali na kusema kuwa ametoa adhabu hiyo kwa kuridhika na ushahidi uliotolewa na ushahidi tosha tosha juu ya washitakiwa hao waliofanya mauaji ya kinyama ya kukusudia.

Awali ilidaiwa kuwa washitakiwa hao walifanya mauaji hayo ya kukusudia usiku wa kuamkia Desemba 1, mwaka jana huko Bukombe mkoni Shinyanga.

Mtoto huyo aliweza kuuliwa na washitakiwa hao na kasha kuondoka na badhi ya viungo kutoka kwenye mwili wa motto huyo.

Kesi hii ni kati ya kesi zilizokuwa zinasubiriwa hukumu kwa hamu na watanzania wealio wengi kwa kungojewa hukumu na ni muendelezo kati ya kesi zinazoendelea kusikilizwa katika mahakama hiyo juu ya mauaji ya kikatili ya kuua albino kiholela yaliyofanyiwa mkoani Shinyannga.


</SPAN>
 
Back
Top Bottom