Watanzania wenzangu, Tujadili hoja na sio mtu

Lami

Senior Member
Jan 1, 2014
117
65
Naomba wote tufahamu kuwa kuna political na professional presidential appointments. Political presidential appointment ni pamoja na ukuu wa mkoa, wilaya, mabalozi, ukuu wa bodi mbalimbali, mawaziri, manaibu mawaziri n.k. Sifa za uteuzi wa nafasi hizi ni nyingi kuziainisha lakini pia ni RAIS atakavyoona inafaa (elimu na ujuzi sio vigezo cha msingi). Mf. Tumewahi kuwa na waziri ambaye ni mtaalamu wa mifupa lakini aliongoza wizara ya Ulinzi.

Professional presidential appointments, pamoja na sifa nyingine nyingi lakini ni lazima Elimu na ujuzi viwe ni vigezo cha msingi. Haiwezekani uwe mtaalamu wa mifupa kisha ukawe katibu mkuu wa wizara ya fedha, HAIWEZEKANI. Ukiwa mtaalamu wa mifupa au fani yoyote ya udaktari subiria ukatibu mkuu wizara ya Afya au ukurugenzi wa halmashauri n.k.

Kwa maelezo hayo mafupi, naomba sote tufahamu kuwa Makonda hakuteuliwa ukuu wa wilaya na baadae ukuu wa Mkoa kwa ajili ya vyeti sababu ukuu wa wilaya na mkoa ni political presidential appointments na sio professional presidential appointment.

Hoja ya vyeti ingetiki sana kama Makonda angekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri yoyote sababu ukurugenzi ni professional presidential appointment sawa na ukatibu wa wizara.

Hoja ya vyeti inashikiliwa bango kwa wingi na wale ambao, kama sio wauzaji wa madawa basi wana maslahi binafsi na mapana katika hayo madawa ya kulevya. NAUOMBA UMMA wa Watanzania, Turudi katika HOJA YA MADAWA YA KULEVYA, Makonda amesaidia kuuwasha Moto, TUMUUNGE MKONO. Kama amekosea approach, basi turekebishe na kusonga mbele katika VITA na sio kujadili kuhusu mtu mmoja mmoja. MADAWA YA KULEVYA NI JANGA!!!!

Nawasilisha.
 
Lazima Gwajima vs F.Mbasha wajadiriwe na SIYO Makonda.
 
Hapa cheti tu
9cb2161a599e01bcfc88df453071a604.jpg
 
Kwanza athletes vyeti,na kama amefoji hana tofauti na wazee wa ngada.
 
Naomba iwe ni mwanao amechukua device yako aka-login JamiiForums na kupost hizo pumba hapo juu wakati huo ukiwa umelala...naamini aliyeyaandika hayo sio mtu mzima aliehangaika kutafuta elimu.
 
Naomba wote tufahamu kuwa kuna political na professional presidential appointments. Political presidential appointment ni pamoja na ukuu wa mkoa, wilaya, mabalozi, ukuu wa bodi mbalimbali, mawaziri, manaibu mawaziri n.k. Sifa za uteuzi wa nafasi hizi ni nyingi kuziainisha lakini pia ni RAIS atakavyoona inafaa (elimu na ujuzi sio vigezo cha msingi). Mf. Tumewahi kuwa na waziri ambaye ni mtaalamu wa mifupa lakini aliongoza wizara ya Ulinzi.

Professional presidential appointments, pamoja na sifa nyingine nyingi lakini ni lazima Elimu na ujuzi viwe ni vigezo cha msingi. Haiwezekani uwe mtaalamu wa mifupa kisha ukawe katibu mkuu wa wizara ya fedha, HAIWEZEKANI. Ukiwa mtaalamu wa mifupa au fani yoyote ya udaktari subiria ukatibu mkuu wizara ya Afya au ukurugenzi wa halmashauri n.k.

Kwa maelezo hayo mafupi, naomba sote tufahamu kuwa Makonda hakuteuliwa ukuu wa wilaya na baadae ukuu wa Mkoa kwa ajili ya vyeti sababu ukuu wa wilaya na mkoa ni political presidential appointments na sio professional presidential appointment.

Hoja ya vyeti ingetiki sana kama Makonda angekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri yoyote sababu ukurugenzi ni professional presidential appointment sawa na ukatibu wa wizara.

Hoja ya vyeti inashikiliwa bango kwa wingi na wale ambao, kama sio wauzaji wa madawa basi wana maslahi binafsi na mapana katika hayo madawa ya kulevya. NAUOMBA UMMA wa Watanzania, Turudi katika HOJA YA MADAWA YA KULEVYA, Makonda amesaidia kuuwasha Moto, TUMUUNGE MKONO. Kama amekosea approach, basi turekebishe na kusonga mbele katika VITA na sio kujadili kuhusu mtu mmoja mmoja. MADAWA YA KULEVYA NI JANGA!!!!

Nawasilisha.
Ama hujui kinachomkabili Makonda kiasi cha kumvuruga kwa kiwango kilichothibitika, au umeamua tu kuziondosha kichwani akili zako kwa muda!
 
Makonda kupambana vita ya madawa ya kulevya alikuwa yupo sahihi. ila alishindwa kutumia akili.
Na ndio maana watu walihoji elimu yake.

Na kwanini serikali imlilie makonda tu wakati huo hiyo kazi wapo watu wengi wenye vigezo vyote na wanaweza wakaifanya hiyo kazi vizuri kabisa?
 
Wewe huelewi!!! Hoja kuhusu Makonda sio elimu yake bali kughushi!!! Hata kama angekuwa amemaliza darasa la 7 hakuna tatizo... tatizo kufoji!! Muhongo ametuambia kwamba Ole Sendeka alipata ZERO Form VI; umeona kuna mtu anahoji kuhusu Sendeka?!

Nyie watetetezi wa Makonda mbona mna vichwa vigumu kuelewa?!

Acheni kutetea ujinga! Forgery ni kosa la jinai!!! Hoja yenu ibaki kwamba Makonda hajafoji vyeti lakini mnavyoongea kwa namna ya kukubali kwamba amefoji vyeti lakini mnaona hakuna tatizo inaonesha hamfahamu mnachoongea!!!

Kama kweli amefoji amekiuka moja ya misingi ya maadili ya kiongozi (sio mtumishi) wa umma! Aidha amekiuka ahadi ya kwanza ya kiongozi wa umma!!
 
Amekutuma umtetee si alilianzisha mwenyewe. Yeye aweke vyeti tu ndio kitu pekee cha kujinasua na hili. Vyinginevyo hata wewe hujui unalongo ongea. Hawa jamaa wamenyanyasa sana watumishi therefore watu wana chuki sana zidi yao. Panda chuki vuna hasira. Ngoja akomeeeeeeeeee! Na chakumsaidia ni kuweka vyeti tu porojo za nini?
 
Pumbavu kweli, rais mwenyewe alisema kama cheti chako cha darasa LA sabaa utafanya kazi ya darasa LA saba iweje yeye? Kuna mambo ya kutetea.
 
Mleta mada unaifahamu elimu ya Mh.Bulembo?Nani ulimsikia anahoji uteuzi wa Bulembo kuwa mbunge?Hoja inayojadiliwa juu ya Daudi ni jinai aliyoifanya kwa kuiba cheti na jina la mtu na si madaraka aliyonayo.Hata asingekuwa amesoma walau darasa la kwanza,bado waliomteuwa wangeweza kufanya hivyo na hakuna ambaye angewapinga.

Hatuna tatizo na nafasi yake wala utendaji wake,kiutendaji ni kijana mzuri mwenye uthubutu,hilo halina ubishi,ni mwendawazimu pekee anayeweza kuupinga uthubutu na ujasiri wa Daudi,tatizo lake ni moja tu,alilidanganya Taifa juu ya Elimu yake,hilo ndilo tatizo.

Akijitokeza hadharani na kuusema Ukweli,tupo tutakaomsihi mh.Rais amsamehe kwa niaba yetu udanganyifu alioufanya,na amuache aendelee na nafasi yake Kama Daudi Albert Bashite mwenye "F " za kutosha kidato cha nne lakini mwenye "PhD" ya ujasiri na uthubutu katika uongozi wake.Kuendelea kujiita Paul Christian Makonda,huku akijuwa si majina yake na wala sifa za kielimu alizonazo si zake hakuwezi kumfanya asijadiliwe.Labda akahifadhiwe jeshini na kugeuzwa "kifaa cha jeshi", vinginevyo hakuna Riwaya yoyote itakayoweza kutufanya tusihoji uadilifu wake kitaaluma.
 
Huku kwetu kuna jamaa aliiba gari mkoa mwingine akaja nalo huku kwetu akawa anatamba nalo na pia wakati mwingine akawa anatusaidia mfano ukiwa na mgonjwa ukimwomba msaada kumpeleka mgonjwa wako alikuwa anasaidia kuna siku kwa kutumia gari lake alifanikiwa kuwadhibiti majambazi waliokuwa na silaha lakini baadae ikagundulika kuwa gari hilo lilikuwa la wizi sasa sijui tuwaombe polisi wamfutie kesi ya wizi wa gari hilo maana alikuwa anatusaidia sana na hilo gari na pia alisaidia kukamatwa kwa majambazi yenye silaha ambapo bila yeye majambazi hayo yangeleta madhara makubwa
 
Wewe elimu yako mbona haikusaidii kutwa kucha mtandaoni wakati choo chenu cha shimo kimezungukwa na nyasi ndefu,hata simba mnyama aweza winda swala humo
 
Back
Top Bottom