Watanzania wenzangu tufanye mabadiliko

Watanzania wenzangu tufanye mabadiliko

mkezwag

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2011
Posts
3,245
Reaction score
1,080
Tumekuwa na ccm na wazazi wake (TANU na ASP) kwa miaka 54 sasa toka tupate uhuru mnamo December 9,1961.Tumekuwa tukiichagua ccm yenye watu wale wale na sera zile zile kwa miaka 35 sasa.

Mwalimu Nyerere tangu alipowaambia watawala wetu kwamba watanzania wanataka mabadiliko ni zaidi ya miaka 14 sasa na hakuna lililofanywa na ccm mpaka wananchi tulivyoamua kufanya hayo mabadiliko miaka miwili iliyopita kupitia rasimu ya pili ya katiba mpya,hata hivyo ccm walituchakachua, wakiongozwa na samwel Sita na samia kwa kuwa hawakutaka tufanye mabadiliko.Leo tumeamua kutaka kufanya mabadiliko kwa njia ya kura ccm na mgombea wao Magufuli na samia( aliyeongoza wenzake kutunyima mabadiliko kupitia katiba mpya) sasa wanajifanya wanaweza kutuongoza kwenye mabadiliko tunayoyataka-UONGO HUU,wanakuja na propoganda lukuki kwa kutumia watu tofauti tofauti lakini yote ni uongo

Mwananchi wa Tanzania nakuomba orodhesha mambo ambayo ukawa wanaahidi kutufanyia likiwemo suaLa la katiba mpya tukiwapa kura,then wape kura yako.Kwenye uchaguzi wa 2020 kazi yako ni moja tu kuangalia kama mambo hayo yametekelezwa au laa.Kama yametekelezwa utawapa kura yako tena hiyo 2020 kama hayajatekelezwa usiwape kura.

TANZANIA NI ZAIDI YA CCM NA NI ZAIDI YA CHADEMA
Tujifunze kuipenda nchi yetu.
JK aliahidi kujenga reli ya kati,Je imejengwa?
Aliahidi kuifanya kigoma kama Dubai imekuwa hivyo?

Hiyo ni mifano michache tu,Chukua daftari lako,pitia kile ulichooahidiwa ten years ago kama hakijafanyika,SEMA NO KWA CCM,haijarishi wewe ni mwanachama au siyo.
ACHA KUPIGA KURA KWA MAZOEA.Kura yako inadhamani sana kwa nchi yako na familia yako
 
Watanzania wengi hatufahamu kuendelea kuipa CCM nguvu ya kutawala ni sawa na kuiuza nchi hii, ni sawa na kuwanyima haki za msingi Watoto na wajukuu Zetu.

Tunapaswa kujua Palipo na mashindano ndipo yalipo maendeleo, natafakari na wazua najiuliza vipi kama Mobitel (kwasasa tiGO) wangeendelea kuwa mtandao pekee wa huduma za simu Tanzania. Bila shaka mpaka leo tungekuwa tunaongea kwa tsh 350/sekunde na sms moja ingekuwa tsh 200

Ushindani ulileta unafuu wa mawasiliano, nchi hii inahtaji ushindani wa uongozi wa vyama katika nchi, ili chama kimoja kikiharibu kijue kesho sina changu.

Lazima tuistiri nyumba yetu Tanzania, neema ya nchi hii ipo katika mikono yangu na yako. Tukubali kubadilika.

Huwa nakaa na watu hapa kijijini nilipo nawauliza jamani "mimi nina mshahara na kazi nzuri, natibiwa na bima ya Afya kwa mshahara wangu na watoto wangu" na bado nahtaji mabadiliko, vipi ninyi mnaoamka asubuhi hamjui kesho yenu? hata ukiumwa hospitali hutibiwi

Watoto wenu wanaenda shule na nguo zimechanika, mazao yenu hayana soko la uhakika, umeme kwa biashara zenu si rafiki, ushuru kwa mazao yenu ni sumu, na bado mnaendelea kuikumbatia CCM?

Watanzania tuamke, Historia itatukumbuka. Waelimishe ndugu na jamaa zako na marafiki, umuhimu wa mabadiliko ya kidemokrasia.
 
Sawa lakinı hawa wengne ndo kabisa msiba.Umkabidhi nchi Lowasa na Mtei family utarajıe masikini wa Nangurukuru,Buhigwe,Mafia,Mbozi na Goziba wakombolewe???Akah,nafuu CCM watajisahihisha.
 
Sawa lakinı hawa wengne ndo kabisa msiba.Umkabidhi nchi Lowasa na Mtei family utarajıe masikini wa Nangurukuru,Buhigwe,Mafia,Mbozi na Goziba wakombolewe???Akah,nafuu CCM watajisahihisha.

CCM wajisahihishe?, Thubutu! Hatuhitaji KAKAKUONA wala PWEZA wa Ujerumani, safari hii kombe linakwenda MONDULI-Masaai Yerro Subhai
 
Kwa hili nakuunga mkono asilimia 100,na pia naendelea kutoa rai kwa washabiki kuwa kuwaza hata nusu dakika juu ya mustakabali wa nnchi yako,na usijiangalie mwenyewe anglia na wenzio,kwasababu wewe umeshiba unaona raha mwenzio akiwa na njaa,sis wote ni ndugu lazima tupendane na tuhurumiane,mimi binafsi naamini kuwa hakuna chama kitachokuja kugawa hela kwa wananchi bila kufanya kazi,ila ila naamini kitasimamia rasilimali zetu kwa haki na uwazi,pia kitaboresha huduma. Muhimu kama. Vile maji sari na salama afya bora kwa upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa. Bei nafuu,uchumi imara kwa kuwekeza. Zaidi kwenye. Kilimo chenye tija na viwanda vidogo vidogo na vikubwa,pia elimu kuwa na elimu bora kwa bei nafuu bila kusahau gharama vifaa vya ujenzi ili kupata nyumba bora na imara kwa kila mwananchi,yote yanawezekan kwanza kwa kuwa na mtazamo chanya kuhusu mabadiliko.
 
Twende na mabadiliko 2015, kwani ccm haiwezi kubadilika miaka yote, wamezoea kufanya kazi kwa mazoea, huo ndo utamaduni wao.
 
team lutheran at work
wewe ni bonge laboga na seeeenge rema kweli kweli aliye kudanganya kuwa wote tuna muamini yesu ni nni haya mambo ya kupenda sana kuleta chuki za kidini ccm mtakuja juta siku siyo nyingi ! Mmejaribu kwetu waislamu mmegundua tumesha wajuwa na kura zetu hampati mmeamua kugeukia kwa walutheran mungu atawalaani!
 
Sawa lakinı hawa wengne ndo kabisa msiba.Umkabidhi nchi Lowasa na Mtei family utarajıe masikini wa Nangurukuru,Buhigwe,Mafia,Mbozi na Goziba wakombolewe???Akah,nafuu CCM watajisahihisha.

Unahtaji kuwa nafikira pana zaidi ya hiyo, ujue kwanza how the system works, na sio kuja na maneno mepesi kiasi hiki?

Huko ccm mbona tangu mtu kiongozi mkuu wa nchi mpka wanae wanakula nchi hii bila huruma na husemi?

Tuambiwe meremeta ni ya mtei?
Escrow ni ya Lowasa?
Walificha pesa Stanibic ni wafuasi wa vyama vya UKAWA?
Ebu acha fikira duni Mtanzania mwenzangu, usione watu wanasema bora Shetani kuliko CCM hii na ni kiwango cha juu kabisa cha Kukata tamaa kuonesha jinsi CCM ilivochezea maisha yao kwa ahadi Bandia.
 
Back
Top Bottom