Watanzania wengi ni kweli hawajui kuandika na kusoma, thats true.
Ilikuwa ni aibu sana kwenye kuandikisha vitambulisho vya uraia maeneo ya vijijini.
Hapa wilayani kwangu (mkoa wa Iringa) ambapo makao makuu ya wilaya yapo kilometa 4 nilishangaa mpaka nkaishiwa mshangao kuona mamia ya watu hawajui kuandika.
Kumbe inaonekana watu walishindwa kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwa sababu hiyo.
Sasa kwenye uraia hawakuwa na vitambulisho hivyo, wakalazimika kuandika barua ambayo inasainiwa na mwenyekiti wa kijiji. Mwanzoni mwenyekiti akawa anawaandikia ila wakawa wengi sana hivyo mwenyekiti alichoka, akaandika barua moja akaibandika ili kila mtu akopi, cha ajabu watu walishindwa kukopi, wakabaki wanasubiri msaada wa kuandikiwa.
Wote kuanzia bodaboda mpaka wazee.