Watanzania wengi hawajui kuandika

Watanzania wengi hawajui kuandika

kibunange

Senior Member
Joined
Feb 18, 2015
Posts
165
Reaction score
148
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali kwenye mitandao na maeneo mengi na nimegundua watanzania wengi hawana mbinu za uandishi eidha kwa makusudi au kwakutokujua mfano:

Fedha=feza
Thamani=Samani
Mpira=Mpila
Teremka=Telemka
Basi=Bax

Pia wengi wamekuwa wakiandika jumbe ambazo mwishowe hazileti maana au mantiki na hivyo kumfanya msomaji kupuuzia ujumbe husika. Kunatakiwa jitihada kubwa sana kuwasaidia vijana kuweza kuandika kwa ufasaha.

Asanteni tujirekebishe
 
Sio kwamba hawajui,bali wanachukulia poa tu.
Pia language budget ndo maana mtu anaandika vyovyote akijua wazi wataelewa hata akiandika herufi tofauti.
 
Watanzania wengi ni kweli hawajui kuandika na kusoma, thats true.
Ilikuwa ni aibu sana kwenye kuandikisha vitambulisho vya uraia maeneo ya vijijini.
Hapa wilayani kwangu (mkoa wa Iringa) ambapo makao makuu ya wilaya yapo kilometa 4 nilishangaa mpaka nkaishiwa mshangao kuona mamia ya watu hawajui kuandika.
Kumbe inaonekana watu walishindwa kujiandikisha kwa ajili ya kupiga kura kwa sababu hiyo.
Sasa kwenye uraia hawakuwa na vitambulisho hivyo, wakalazimika kuandika barua ambayo inasainiwa na mwenyekiti wa kijiji. Mwanzoni mwenyekiti akawa anawaandikia ila wakawa wengi sana hivyo mwenyekiti alichoka, akaandika barua moja akaibandika ili kila mtu akopi, cha ajabu watu walishindwa kukopi, wakabaki wanasubiri msaada wa kuandikiwa.
Wote kuanzia bodaboda mpaka wazee.
 
hao wanajua kuandika, sema hawafati kanuni za uandishi na kuandika kwa ufasaha.

Tembekea benki siku moja utacheka mtu yuko smart ila anakuomba umsaidie kuandika (kujaza) taarifa zake.

kundi kubwa hawajui/hatujui ama tunapuuza kuandika kwa ufasaha, huku kundi kubwa zaidi likiwa halijui kabisa kuandika hata A na a (soma A kubwa na a ndogo)
 
Kwa muda mrefu nimekuwa nikifuatilia mijadala mbalimbali kwenye mitandao na maeneo mengi na nimegundua watanzania wengi hawana mbinu za uandishi eidha kwa makusudi au kwakutokujua mfano:

Fedha=feza
Thamani=Samani
Mpira=Mpila
Teremka=Telemka
Basi=Bax

Pia wengi wamekuwa wakiandika jumbe ambazo mwishowe hazileti maana au mantiki na hivyo kumfanya msomaji kupuuzia ujumbe husika. Kunatakiwa jitihada kubwa sana kuwasaidia vijana kuweza kuandika kwa ufasaha.

Asanteni tujirekebishe

Hilo neno kwenye red limeandikwa kwa ufasaha?
 
Hapo kwenye thamani na samani yupo sawa kbsa ila ni muktadha tu ndiyo unaweza kutofautisha.
Samani inatumika ktk vitu km vile meza, viti n.k
thamani hasa ktk viumbe na vitu pia.
Mfano.
Ww ni wa thamani sana kwangu. Kwahiyo huwezi sema ww ni wa samani sana kwangu.
Neno jumbe siyo sahihi ni ujumbe. Hakuna wingi wa neno ujumbe.
Pia hatuna neno eidha ktk lugha ya kiswahili
 
hao wanajua kuandika, sema hawafati kanuni za uandishi na kuandika kwa ufasaha.

Tembekea benki siku moja utacheka mtu yuko smart ila anakuomba umsaidie kuandika (kujaza) taarifa zake.

kundi kubwa hawajui/hatujui ama tunapuuza kuandika kwa ufasaha, huku kundi kubwa zaidi likiwa halijui kabisa kuandika hata A na a (soma A kubwa na a ndogo)
Tofautisha kushindwa kujaza taarifa na kutojua kuandika.
Kwahiyo mtu kukuomba umsaidie kujaza taarifa haimanishi hajui kusoma na kuandika. Ni lugha tu hasa hiii ya kigeni inaleta mkanganyiko.
 
Back
Top Bottom