Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Heshima kwenu wana jukwaa hili, Mungu muumba wa vyote atupe rehema.
Binadamu tumepewa utashi wa kutambua mambo yaliyo mabaya na mema kwa mujibu wa vitabu vitakatifu
Kwa utashi huo huo, hutokea baadhi yetu kuungana katika kusimamia au kudai jambo fulani.
Kwa kuwa tuna utashi wa kutambua jambo gani baya au jambo gani jema , hivyo basi hatuna budi kabla ya kuunga mkono jambo fulani kulitafakari kwa kina ili kuepuka kutoutendea haki utashi wako uliopewa kama zawadi na Mungu.
Hivi karibuni na hata sasa, vijana wengi hasa huku mitandaoni tumekuwa washabiki wakushabikia mawazo au mtazamo wa mtu fulani pasipo kutumia utashi wetu kupima hicho tunachotaka kushabikia ilimradi tu kimetoka au kuanzishwa na mtu /kiongozi unayemuamini.
Matokeo ya haya mambo ya kudakia jambo hewani pasipo kulitafakari na kutafuta mikakati madhubuti ya kulisimamia, mara nyingi huishia hewani pia hata kama lingeleta matokeo chanya kwa jamii.
Hebu tupitie mifano michache iliyodakwa hewani na baadae kuishia hewani au kuelekea kuishia hewani ;
1. Swala la kijana anayedaiwa kutoweka /kupotea Ndg Ben Saanane - hili naamini wengi tulilidaka hewani na kwa sasa tumekosa tusimamie wapi kwani hatujui undani wake.
2. Swala la UKUTA - hili lilitangazwa na kuanzishwa mara kadhaa na liliposemwa watu wengi walilipokea kwa hamasa lakini sasa hivi hakuna anayejishughulisha kufahamu kilichosababisha liishie hewani
3. Ahadi ya mikopo kwa wanafunzi wa vyuo Vikuu - wakati wa kampeni, hii ilikuwa ahadi kubwa na ya matumaini. Lakini sasa, baada ya kutotekelezwa kwa ahadi hii hakuna anayeshinikiza wala kuchukua hatua kuidai kwani ahadi ni deni na kauli ya kiongozi ni sheria.
4. Michango ya maafa kagera - watanzania kupitia nyumba za ibada, makundi ya wafanyabiashara na wahisani walihamasishwa na kuaminishwa kwamba wanawasaidia wenzao wana Kagera, mambo yalipobadilika hakuna aliyechukua hatua
5.Kusitishwa kwa nyongeza za mishahara na promosheni kwa watumishi wa Umma - wafanyakazi wanaishia kulalamika bila kuchukua hatua ambazo zingewasaidia. Huenda walilidakia hewani na tunavyolichukulia sivyo lilivyo ndio maana hata wanao lalamika wanalalamikia hewani badala ya mahali husika.
6. Ongezeko la 15%ya bodi ya mikopo kwa wanufaika - wakopaji wakati wanakopa waliambiwa watarejesha kwa makato ya 8%,leo makubaliano yanakiukwa hakuna anayechukua hatua badala yake wote wanalalamikia hewani!! Pia huenda nalo tumelidaka hewani ndio maana hata wahusika nao wanalalamikia hewani badala ya mahali husika.
Yako mengi sana tena sana! Na wewe ongeza ya kwako.
Mimi naona kweli bora Malaika ashuke azime mitandao yote huenda tutabadilika kutoka kulalamika hewani hadi kuchukua hatua stahiki.