Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,948
Tuliwaondoa wakoloni kwa sababu tulitaka kuwa watu huru wa nafsi. Watu wanaoweza kufikiri na kutenda kwa uhuru yale wanayoyataka.
Tulitaka tuwe huru kuwahoji na kuwadhibiti viongozi wetu. Tulitaka tuwe na uwezo wa kuwaadabisha viongozi wanaotenda kinyume na matakwa yetu, n.k.
Hatukudai uhuru kutoka kwa mkoloni ili tuwe kwenye ukoloni wa mtu au watu weusi. Ukoloni siyo rangi bali ni falsafa ya kiutawala.
1) Ukilinyima Bunge uhuru wake, ukaamua hata kuwatishia wabunge wanaowatetea wananchi, wewe ni mkoloni tu, hata kama ni mweusi na unaimba nyimbo za uzalendo. Mkoloni hakutaka uwepo wa bunge huru lenye uwakilishi huru wa wananchi.
2) Ukiwanyima watu kufanya siasa, hata kama wewe ni mweusi, wewe ni mkoloni tu. Mkoloni kwa sababu ya hofu ya siku moja kuondolewa kwenye madaraka, alizuia harakati za kisiasa kupitia makundi mbalimbali. Alizuia wasomi kushiriki harakati za kisiasa.
3) Ukivinyima uhuru vyombo vya habari na kuvitengenezea sheria za kuvigandamiza, wewe hata kama ni mngoni, wewe ni mkoloni tu. Mkoloni alizuia magazeti yaliyoonekana yana mwelekeo ya kuwaelimisha watu juu ya umuhimu wa watu kuwa huru.
4) Ukiwanyima watu haki ya kukosoa, haki ya kuhoji viongozi wao, wewe ni mkoloni tu hata kama wewe ni mkara. Mkoloni hakutaka kukosolewa na watawaliwa. Aliweka mifumo ya kuwadhibiti wakosoaji wote.
5) Kama unawakamata watu hovyo kwa nia ya kuwatia watu hofu ili watu wasihoji mapungufu yako, wewe ni mkoloni tu, hata kama wewe ni msukuma, utakuwa mkoloni tu. Mkoloni aliwafunga wanaharakati, aliwafunga wapigania uhuru, aliwaua babu zetu waliokuwa wakipigania uhuru. Nia ni kutaka kuwatisha na kuhakikisha hakuna anayesumbua utawala wa kikoloni.
6) Ukaamua kuendesha mambo kwa kuwapendelea watu wa kabila fulani, au kanda fulani au chama fulani au dini fulani, wewe ni mkoloni tu, hata kama unakijua sana kindengereko. Falsafa ya wakoloni ilikuwa kutenganisha watawaliwa ili wasiwe na umoja dhidi ya mtawala mkoloni.
Watanzania wahakutafuta uhuru ili wawe na reli, barabara, ndege, hospitali, meli, na umeme, lakini waendelee kuwa watawaliwa wa fikra na nafsi zao. Vitu na huduma ni matokeo ya uhuru na wala vitu hivyo huviwezi kugeuka na kuwa ndiyo uhuru tulioutafuta.
Watanzania, tutakuwa tunawaenzi majemedari wetu, walioanzisha harakati za kuupata uhuru kwa kutokubali kabisa kupokonywa uhuru ambao tayari ulipatikana.
Tuwakumbuke Chifu Mkwawa, Chifu Isike, Chabruma, Mirambo, Kawawa, Nyerere, Bibi Titi na wengineo. Hawa walisimama kidete siku zote, wengine walikubali hata kupoteza maisha yao kwa nia ya kuulinda na kuutafuta uhuru.
Ni lazima Watanzania tuulinde uhuru wetu dhidi ya mkoloni yeyote bila ya kujali mkoloni huyo ni Mzungu, Mchina, Muamerika au Mwafrika mweusi kama sisi.
Mkoloni ni mkoloni tu. Ukoloni siyo rangi wala siyo utaifa bali ni falsafa. Yeyote anaweza kuwa mkoloni bila ya kujali rangi yake. Na mkoloni wa rangi yako ni hatari zaidi maana unaweza kuchelewa kugundua kuwa ni mkoloni, kwa sababu ya fikra zilizozoeleka kuwa mkoloni ni lazima awe na ngozi nyeupe.