figganigga
Platinum Member
- Oct 17, 2010
- 26,662
- 59,099
Watanzania waishio nchini Afrika Kusini wamefanya maandamano makubwa mjini Johannesburg leo Novemba 5, 2025 wakipinga mauaji ya raia yaliyotokea nchini Tanzania kufuatia matukio ya kisiasa ya hivi karibuni.
Waandamanaji hao wamesema wanashindwa kuvumilia kuona nchi yao ikipoteza maisha ya watu wengi wasio na hatia, wakidai kuwa mauaji hayo yametekelezwa kwa amri ya viongozi wa juu serikalini.
Wakiwa wameshika mabango yenye ujumbe wa “Stop Killing Tanzanians”, “Justice for Victims” na “Samia to ICC”, Watanzania hao wamewasilisha madai matatu makuu kwa jumuiya ya kimataifa:

- Uchaguzi wa Oktoba 29, 2025, ufutwe kwa madai kuwa haukuwa huru wala wa haki.
- Rais Samia Suluhu Hassan ashtakiwe katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kwa kuhusishwa na mauaji ya raia.
- Katiba mpya itungwe ili kurejesha misingi ya haki, demokrasia, na uwajibikaji nchini Tanzania