Watanzania waishiao Kenya,wanachaniwa vibali vya kuingia Kenya na polisi bila sababu, na kusingiziwa kuingia kinyume

britanicca

JF-Expert Member
May 20, 2015
15,636
30,004
Mtanzania Anthony ***** aishiye Ngara road Kenya amesema kwa siku za karibuni polisi wa kenya wamekuwa wanatumia nguvu na ubabe sana pindi wanapokutana na watanzania,

Watanzania wanaofanya kazi Kenya wanalalamika kwamba mpaka sasa watanzania 13 wameshakamatwa na askari na. kutozwa hela kiholela, saa nyingine wanayachana makusudi makaratasi ya kumruhusu watanzania kuwa Kenya ili wamsingizie yupo nchini kinyume cha sheria,

"Ukiwakuta njiani ukawaonesha vibali wanakishikiria wanasema tuoneshe yellow fever card kama unayo wanauliza leta hotel uliyobook, kila kitu kikiwa sawa wanasema permit yako si valid ni fake,.ukikataa wanichana na kupoteza ushahidi ili uonekane umeingia nchini kinyume, na ukishapelekwa kituoni mpaka ujieleze wakuelewe so leo,"

Anatoa usharui kwa watanzania "kuwa makini wawapo njiani au wanapotembea usiku, au wanavyopanga nyumba wasiji expose sana kwa majirani maana hutoa taarifa kwa polisi wale nao hela,"
 
Warudi tu nyumbani. Lete hizo pesa fungua biashara hapa. Niliwahi kukutana na wengine miaka 7 iliyopita wakilalmikia hali hii ya polisi kuchukua pesa hasa ukiwa na biashara. Ukikataa walivyoeleza wanaleta msokoto wa bangi na kukubambikia. Walisema hawatakaa warudi tena. Kama ndio umeenda fikiria tena. Ndio hali halisi
 
Police wa kenya wanapenda sana Rushwa wako tayari wamwachie gaidi kwa sababu ya pesa

Kenya ni nchi ya ukabila sana watanzania ubqguliwa sana isipokuwa wamasai

kukamatwa kenya ni jambo la kawaida sana hasa kwa watanzania wasudani Na wasomalia
Kweli.kabisa nasikia hata alshabaab wanawaachia kwa rushwa
 
Wameanza kumwaga ugali ngoja sisi tuje tumwage mboga tuzime na moto na jikoni tulowanishe maji kabisa hakuna kupika tena
Mtanzania yupi leo anaweza kumwaga mboga kwa wakenya?? Sisi tumefundishwa woga vichwani mwetu kila siku tunaambiwa TANZANIA ni kisiwa cha amani huku tukiishi chini ya mwamvuli wa woga
 
Wakichana passport watakuwa wanatafuta balaa lingine. Kuna yale maneno ndani ya passport sio mepesi.

Sent from my iPhone using JamiiForums
Wakichana usidhani wanaonesha kwamba wanachana hadharani, wanaichana na unatiwa selo
 
Mtanzania Anthony ***** aishiye Ngara road Kenya amesema kwa siku za karibuni polisi wa kenya wamekuwa wanatumia nguvu na ubabe sana pindi wanapokutana na watanzania,

Watanzania wanaofanya kazi Kenya wanalalamika kwamba mpaka sasa watanzania 13 wameshakamatwa na askari na. kutozwa hela kiholela, saa nyingine wanayachana makusudi makaratasi ya kumruhusu watanzania kuwa Kenya ili wamsingizie yupo nchini kinyume cha sheria,

"Ukiwakuta njiani ukawaonesha vibali wanakishikiria wanasema tuoneshe yellow fever card kama unayo wanauliza leta hotel uliyobook, kila kitu kikiwa sawa wanasema permit yako si valid ni fake,.ukikataa wanichana na kupoteza ushahidi ili uonekane umeingia nchini kinyume, na ukishapelekwa kituoni mpaka ujieleze wakuelewe so leo,"

Anatoa usharui kwa watanzania "kuwa makini wawapo njiani au wanapotembea usiku, au wanavyopanga nyumba wasiji expose sana kwa majirani maana hutoa taarifa kwa polisi wale nao hela,"
Acha uchochezi wewe.
 
Back
Top Bottom