hii video nimetumiwa,jamaa huko mwanza kajirusha alikuwa
Kwenye daraja la mabatini
Chanzo inasemekana mambo ya mapenzi
Tukirudi kwenye hiyo video ukiangalia,wakati yuko juu watu wanampita hawana hata habari naye hakuna hata mtu anafanya maamuzi ya kumzuia
Ukija huko chini napo mijitu imekaa ikimshangaq tu wamemgeuza sinema utafikiri wanangalia tamthiliya zao zile za kituruki
Mbongo sahvi utu, ubinadam umepotea roho mbaya na ukatili unawaingia tu
Ndomana tunaonaga matukio mengi ya ajali mtu akipata watu wanachofanya kwanza ni kjku record tu msaada hakuna
Ova
Pole sana. Naona umeguswa na kukerwa na Watanzania. Pole.
Walakin, suala hili ni zito na gumu kwa binadamu yeyote yule.
Sasa wewe unadhani kwa kuangalia Video na tukio hilo moja, unaweza kuishutumu Nchi nzima kuwa ni jamii katili na linalopoteza Ubinadamu ni sawa kweli?
Tambua, hakuna aliyeshuku kijana huyo atajirusha na hilo limesemwa na walioshuhudia mkasa/tukio hilo, tena huku wakiwa wanasikitika. Sasa wewe umeenda mbali na kiujumla jumla kuishutumu Nchi Nzima kwa msingi wa tukio hilo moja?
Mrangi, badala ya kutoa lawama ungeomba vyombo husika kuhimiza watu kuwa na ufahamu wakaribu zaidi na wale wa karibu nao kugundua dalili za unyogovu, hilo linaweza kusaidia na kuepusha majanga na matukio kama hayo kwenye Jamii.
Unafikiri ni njia zipi zinaweza kutumiwa kuboresha afya za watu (mental health)kama kijana huyo?
Kama itakupendeza, naomba kuwaombea samahani Watanzania wote kwa yaliyokusibu.
NB: Tujaribu kuepuka na kauli hizo pana, hazileti tija kwa Jamii wala Nchi.