Mchokoo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2015
- 1,179
- 1,579
Ni kweli tumenyimwa pesa na wahisani kwa sababu ya kuikandamiza demokrasia!
Tena ni kweli kwamba imetuuma sote hata kama tunajifaragua kuwa hatujari.
Ni kweli pia sote tunaenda kuwa wahanga wa mtego huu hatari bila kujali waliokuwemo na wasiokuwemo!
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba kwanini tumeamua kuichagua njia ya maneno ya jeuri ilihali tunafahamu fika kuwa hawa wazungu hatuwezi kupambana nao?
Mnaposema wahisani waondoke waende zao!
Waende wapi wakati dunia leo ni sawa na kijiji kidogo tu!
Tazama wao ndio wanapanga bei za malighafi zetu zote!
Wakisema bidhaa zetu zisinunuliwe, hazitanunuliwa, tunataka hilo ama hatulitaki hiyo haijarishi.
Korea ya kaskaz na jeuri yao yote ile ya kujitegemea lakini bado laia wao wanaumia sana kwa sababu ya vikwazo vya hawa jamaa!
Nenda Zimbabwe kwa mzee Mugabe uone matunda ya jeuri ya kimaskini, huwezi hata siku moja ukatamani kile kinachoendele nchini kwake!
Nia yangu si kuwatisha wale wenye maono ya kujitegemea ghafla, ila ninaona kuwa kadri misaada inavyoendelea kukatwa na wahisani wengi wetu ni kama wanapata ujasiri kuvurugikiwa. Huku wakiendelea kuropoka maneno yanayoweza kutufanya kama taifa kuiendea njia ngumu zaidi; hasa pale tutakapoona aibu kurudi nyuma kutoka katika kushupaza shingo kwetu!
Hebu tujitahidi kuwa watulivu, Wapole, na wasikivu ili tusije kubomoa hata kile kidogo tulichokijenga kwa zaidi ya nusu karne sasa!
Mungu ibariki Tz