Uchaguzi 2020 Watanzania tuwakatae CHADEMA na uzushi wao

herzegovina

JF-Expert Member
Oct 28, 2015
3,085
2,000
Salaam,

CHADEMA wamekuwa na tabia ya kumzushia mambo mengi mabaya Rais wetu na mgombea wa CCM. Mfano jana eti wamezusha kuwa rais wetu alizomewa kule Kagera. Cha kushangaza hata video za kuonyesha tukio hilo hazionekani. Rais Magufuli ni kipenzi cha wana KAGERA na wanamwelewa sana ndio maana hata wanafunzi kuanzia chekechea hadi sekondari ilibidi "watoroke" mashuleni wakajae kwa wingi ili kumsikiliza kipenzi chao.

Huu ni mwendelezo tu wa uzushi wao. Chama hiki ni cha kuzusha zusha tu. Kipindi hiki cha kampeni wamezusha kuwa eti "ndege za Magufuli" hazina faida. Huu ni uzushi mkubwa sana. Ndege hizi zimeingiza faida kubwa kwa nchi kwa kusafirisha nyama za mbuzi kwenda mashariki ya Kati.

Pia wamezusha kuwa uwanja wa ndege wa Chato eti hauna manufaa yoyote kwa umma. Je, hawajaona Museveni akitua kusaini mkataba pale? Hawaoni kuwa hata wanyonge wa Vijijini sasa hivi wanaziona NDEGE KUBWA ZIKITUA hivyo kuongeza kipato chao? Lakini hawaoni pia kuwa hali hii ikiendelea basi kila Rais ajaye atajenga uwanja wa ndege KIJIJINI kwake hivyo nchi nzima itajaa viwanja vya ndege na kuwawezesha ng'ombe na mbuzi kuchunga kwenye viwanja vya ndege na hivyo kuiingiza nchi kwenye UCHUMI wa JUU?

Uzushi huu wa CHADEMA unamfanya rais wetu ambaye amejenga VIWANDA 8000 na kutoa Ajira 6,000,000 kwa Watanzania awe mtu wa kupaniki na kufokafoka kwenye majukwaa ya kampeni. Haongelei tena atatufanyia nini Watanzania bali anakuwa anatufokea tu.

WATANZANIA tuwakatae CHADEMA.

Sauti inatosha?
 

Mvumbo

JF-Expert Member
Aug 20, 2015
1,550
2,000
Hakuna tabu kama kimeingia chochote kitu.

1600023575-picsay.jpg
 

NAWATAFUNA

JF-Expert Member
Nov 14, 2019
5,833
2,000
Usihofu mleta mada,watanzania wanatambua kuwa Chadema hawawezi pata kura.ondoa hofu.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
95,837
2,000
yaani ndugu kama unaakili timamuhuwezi kusema hivyo tanzaniaya 61 na ya 2020 unilinganishakweli? mwendawazimu weeeeeeeeee
Wewe ndiye mwendawazimu uliye kubuhu, maana sasa hivi usha kuwa sugu wa matatizo ya ccm.

Miaka 60 tangu uhuru mmetutia umasikini wa kudumu. Hadi leo hii mtanzania hana uhakika wa kesho yake atakula nini?

Alafu jitu linakuja kuisifia ccm! Shame on you
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom