Watanzania Tusijiroge Tena Kwani Katiba Bora Hujiandika Yenyewe Automatically


Mtoto Wabibi

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
451
Likes
286
Points
80
Mtoto Wabibi

Mtoto Wabibi

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2016
451 286 80
Ni maoni yangu
Tusijiroge tena watanzania kuanza kulilia na kushinikiza kuanza upya kwa mchakato wa katiba au kurudia tena kujadili tena rasimu ya warioba kwa kuongeza au kupunguza vitu hasa kwa awamu hii ya tano. TUTAJUTA SANA endapo fisi atakabidhiwa bucha.bora tupige kura kwa rasimu iliyopo japo ina kasoro na tusubiri mpaka katiba itakapojiandika yenyewe kulingana na hali ya nchi.

Kwa nchi yoyote ambayo bado inaendelea na demokrasia haijakomaa vizuri, katiba bora hujiandika yenyewe kulingana na hali ya nchi kwa wakati huo.

Katiba hudai muda wake yenyewe.
katiba nzuri huandikwa wakati nchi imeingia katika mzozo mkubwa wa kiuongozi hasa nafasi za juu za madaraka au endapo kuna serikali ya mseto katika nchi. Vinginevyo katiba itakayoundwa itawabeba walio madarakani(wataamua wao nini cha kuandika na nini cha kuacha kulingana na interest zao kisiasa).Na wengi wa viongizi wa nchi zinazoendelea hutumuia nafasi hiyo kujiongezea mihula/muda wa uongozi kutokana na madaraka na ushawishi wao katika serikali wanazoongoza.

Kwa Tanzania kosa tulishafanya tayari juu ya mchakato wa katiba na mbaya zaidi ilibaki kiporo kwa awamu ya tano.Hivyo ni vizuri tufuate matakwa ya walio madarakani kama ilivyotarajiwa na wengi.Tupige kura ya rasimu ya katiba na kuipa nafasi hiyo katiba ya kujiandika yenyewe kwa nguvu huko mbeleni.Tusubiri tu muda yani iwe miaka mitano,ishirini au hamsini ijayo lakini itatimia tu na muda utanena.

Naamini katiba bora hujiandika yenyewe kulingana na hali ya nchi na sio kwa mashinikizo ya wapinzani au serikali.
By
Mtoto wa bibi
 

Forum statistics

Threads 1,238,772
Members 476,122
Posts 29,330,202